Yatima katika Jamii

By Martha Chimilila

Yatima ni mtoto aliyepoteza Mzazi mmoja ama wazazi wote, inaweza ikawa kwa ugonjwa au kitu kingine chochote.

Tafiti zaonesha kuwa, zaidi ya watoto million 153 ni Yatima kwa kupoteza Mzazi mmoja, na takribani millioni 17.8 wamepoteza wazazi wote wawili. Visababishi vya mtengano kati ya watoto, wazazi na vituo vya kutoa misaada ni umaskini, ukosefu wa mahitaji muhimu kama afya, unyanyasaji wa kijinsia, ulemavu na magonjwa.

‘Chapisho la UNICEF la mwaka 2018 laonyesha zaidi ya watoto million 7.2 duniani wanaishi katika vituo vya misaada na takriban milioni 8.9 wanaishi mitaani. Ongezeko hili la watoto Yatima katika vituo vya kutolea misaada na mitaani inatokana na wazazi wengi kutoweza kuwatunza watoto wao. Maisha duni ya wazazi nchini Latini Amerika, Asia na Afrika pia yaleta athari kubwa katika malezi ya watoto na ukandamizaji wa haki za watoto.

Umuhimu wa kupata matunzo chini ya familia:

Ukuaji chanya wa mtoto na uangalizi mzuri unapatikana katika familia na husababisha matokeo mazuri katika ukuaji na maendeleo ya mtoto. Familia itampatia mtoto upendo, hali ya kukubalika, muingiliano wa kimahusiano na jamii na ushiriki wa kitamaduni.

Kijana mmoja nchini Ethiopia alisema “nilidhani kituo cha kulelea Yatima ndo nyumbani kwetu, sitoweza kutoka na kuishi Maisha ya huko nje. Ila sasa Inabidi nianze kujifunza stadi za Maisha kama kuhifadhi na kudhibiti matumizi ya pesa na mafunzo mengine ambayo ningeweza kupata kama ningelelewa na familia. Hii limesababisha msongo wa mawazo, hisia za kutothaminiwa na kukataa tamaa, jamii hututazama kwa jicho la tofauti sana” chapisho la The Faith of Action Initiative 2014

Watoto ambao wako chini ya uangalizi wa familia au vituo vya misaada wako tofauti sana. Malezi ya kiimani ambayo wanapatiwa yataenenda na jamii inayowazunguka. Imani haihusishi maswala ya dini pekee, la hasha, bali pia mienendo na tamaduni za jamii husika.

Nini kifanyike ili kuondoa tatizo hilo:

Kutengeneza miradi ambayo itasaidia familia duni ili kuweza kuwatunza watoto na kuonesha vyanzo vinavyosababisha msongo wa mawazo kwa wazazi. Kuwekeza katika miradi hii kama vituo vya malezi kwa wazazi wajawazito, vikundi vya kuwasaidia wazazi, vikundi vya kibiashara na mafunzo na huduma nyingi shirikishi zitaweza kupunguza ongezeko la umaskini kwa jamii na mtu mmoja mmoja.

Mpango mzuri wa malezi kwa familia za kulea utakao husisha, uunganishwaji wa watoto kwa familia zao. Hii itasaidia mtoto kuwajua ndugu zake na pia ndugu kuwa na uwezo wa kufatilia mwenendo wa ukuaji wa watoto ambao wako chini ya malezi maalumu au nyumba za misaada.

 “Retrak, ni asasi inayofanya kazi na watoto wa mtaani katika nchini zifuatazo Ethiopia, Malawi na Uganda. Ilitengeneza Taratibu za Uendeshaji kwa kuwaunganisha watoto wa mtaani na familia zao. Taratibu hizi za Uendeshaji zinajumuisha ufafanuzi muhimu na zana kwa kila hatua ya michakato wa uunganishwaji. Hatua hizi zimekua zinafatwa mara kwa mara na hubadilika ili kuweza kufikia lengo lililowekwa na asasi. Retrak kwa mwaka 2009 hadi 2011 iliweza unganisha zaidi ya watoto 600 kwa familia zao” chapisho la The Faith of Action Initiative 2014.

Utoaji wa elimu kuhusu afya ya uzazi mashuleni ili kuweza kupunguza ongezeko la kiwango cha kuzaa kwa mabinti wadogo. Uandaaji wa miradi shirikishi ya kukuza ubunifu na kuvumbua vipaji mbalimbali. Watoto ambao wanaishi katika nyumba za kulelea Yatima wana ndoto nyingi ambazo hawana watu wa kuwashika mkono ili waweze kuzikuza.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *