By Khadija Mbesa
UNHCR Yatoa wito kwa Tanzania Kuacha Kuwaondoa wakimbizi wa Mozambique wanaotafuta Hifadhi.
Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasisitiza ombi lake kwa Tanzania kuacha kuwafukuza kwa nguvu wanaotafuta hifadhi kwa kukimbia vurugu katika mkoa wa Cabo Delgado Mozambique
Ripoti zinasema kuwa, Tanzania imewarudisha Zaidi ya wakimbizi 4,000 mozambique, tangia Septemba. Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa, hii inajumuisha zaidi ya watu 1,500 ambao wamerejeshwa kwa nguvu mwezi uliopita. Kwa sasa wakimbizi hao wamehifadhiwa katika hali mbaya mpakani mwa negomano nchini Mozambique.
baada ya kukimbia mashambulio mabaya na vikundi venye silaha katika mji wa Palma, Matumaini ya wakimbizi hao ya kuweza kupata hifadhi nchini Tanzania yalivunjika kwani Tanzania iliwafukuza na kuwaregesha walipotokea.
Boris Cheshirkov anasema kuwa hali ni mbaya sana kwa akina mama wanaoishi negomano na wasio na familia ya kuwasaidia. Wakimbizi hao wanahitaji maji safi, mazingira masafi ,chakula na huduma za kiafya.
Cheshirkov anasema kwamba, shirika hilo linaomba ushirikiano na Tanzania ili waweze kufika maeneo ya mpakani, na liko tayari kusaidia serikali ya Tanzania kuwapokea wakimbizi hao kulingana na majukumu yao ya kimataifa, huku wakizatiti ya kwamba wana harakati ya kuwawezesha wakimbizi hao wanaokimbia vurugu na mizozo kupata usaidizi, usalama na Huru.