Kwa miaka mingi sana, Nchi ya Kenya imekuwa ikisita kuwapatia wazazi wa kiume haki ya ulezi wa watoto wenye miaka midogo, wakihofia kupuuzwa kwa mahitaji ya mtoto huyo na pia kwa sababu ya propaganda ya, Mlezi we kike anaweza kumlea vizuri mtoto mdogo kuliko mlezi wa Kiume, lakini hayo yote yametupiliwa mbalii baada ya mahakama kuwapa haki wazazi wa kiume, haki ya kulea watoto walio chini ya miaka tisa.
Mahakama kuu imetoa amri ya kuwapa haki wazazi wa kiume ya kulea watoto walio chini ya miaka 9, ikidai kwamba, mujibu wa malezi, haufai kwenda kwa mzazi wa kike mojamoja, hata kama mtoto bado yuko katika umri mchanga.
Ikifwatilia amri hii, Mahakama Kuu imempatia haki mwanaume mmoja anayeishi mjini Nakuru, ya kuwalea watoto wake wawili wachanga, uamuzi huu umeidhinishwa kuwa historia kulingana na kesi zote za ulinzi wa watoto wachanga nchini Kenya.
Malezi ya kisheria ya watoto hao wawili, wenye umri wa miaka 15 na 8, yatagawanywa kati ya baba yao, Alex Njuguna Kagwe na mama yao, Sylvia Mueni Musyoka, Ila kimsingi, watoto hao wataishi na baba yao nchini Kenya.
Sylvia alikimbilia mahakamani, ili kupinga uamuzi huo wa koti, wa kumpatia Alex Njuguna Ulinzi kamili wa watoto hao.
Katika ombi lake, Sylvia alidai kwamba, mahakama ilikosea kisheria ilipokusudia kutoa haki ya kumpa jukumu la malezi Bwana Kagwe, haswa malezi ya mtoto mdogo.
Kulingana na Sylvia, sheria za Kenya zinaweka bayana kwamba, malezi ya mtoto mwenye umri mdogo yanafaa kupewa mama, isipokuwa tu, wakati ulio na hali maalum ya kuamuru vinginevyo.
Ila Kulingana na maslahi bora ya watoto hawa, kwanzia mazoefu yao ya kuishi na baba yao kama mzazi wa kimsingi, na pia umbali wa makaazi ya mama yao ambayo yako Merikani, Mahakama iliamua kutoa haki ya ulezi kwa Baba ya watoto hawa, ikizingatia kwamba, Watoto hawa tayari washazoea maisha ya hapa.
Muhimu zaidi ni kwamba, watoto tayari wamefungamana na Kagwe kama mzazi wa msingi na kuwatoa katika mazingira haya bila shaka kunaweza kusababisha kiwewe cha kisaikolojia.
Mwandishi-Khadija Mbesa