Wazazi katika Hatari ya Kukamatwa kwa kukosa Kusajili Watoto Kidato cha Kwanza

By Khadija Mbesa

“Wazazi ambao hawataweza kuwasajili watoto wao kidato cha kwanza katika mkoa wa Pwani, wako katika hatari ya kukusanywa na serikali” alisema Mkuu wa mkoa wa Pwani bwana John Elungata(RC)

Akizungumza katika kaunti ndogo ya Kinango ya Kwale, Elungata alisema kwamba, serikali haitasita kamwe, katika msukumo wake wa kufanikisha mabadiliko ya asilimia 100 ya kidato cha kwanza kwa watahiniwa wote waliofanya mtihani wa Cheti cha Elimu ya Msingi cha Kenya (KCPE) katika mwaka wa 2020.

Alisisitiza kwamba, wazazi ambao watahujumu sera ya serikali ya mabadiliko ya asilimia 100 ya wanafunzi kuendelea na elimu ya sekondari watashughulikiwa.

RC aliongeza kushinikiza mabadiliko ya asilimia 100 ya wanafunzi, kwa muda mrefu, kutahakikisha nchi inapata kiwango cha juu cha masomo na kuongezeka kwa wafanyikazi walioelimika zaidi.

“Tutalazimika kukwapua mjeledi na kuwakamata wazazi ambao watoto wao hawajajiunga na shule za upili kufikia wiki ijayo” alisema Elungata.

“serikali haitasita katika harakati zake za kuhakikisha watoto wananufaika na elimu ya msingi ya bure na ya lazima” alisema John Elungata.

Alisema kwamba,serikali ya kitaifa, serikali za kaunti na taasisi kadhaa hutoa bursari na udhamini kwa wanafunzi wanaohitaji na wanaostahili na kwa hivyo swala la karo halipaswi kuwa sababu ya wazazi kushindwa kupeleka watoto wao shule ya upili.

Watoto wote, bila ya kujali malezi yao na jamii waliyotokea, wana haki ya kupata shule ya msingi ya bure na shule ya upili ya lazima, hivyo wakikadiria kufanya zoezi la mlango kwa mlango, wakikusanya idadi ya wanafunzi ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza.

Serikali imeazimia kuhakikisha watoto wote wana usawa katika sekta ya elimu, aidha iwe ya msingi, au ya upili.https://www.kbc.co.ke/parents-risk-arrests-for-failing-to-enroll-their-children-in-form-one/embed/#?secret=2w0jajGU9m

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *