Ripoti kutoka kwa shirika la usalama la mtandao limesema kwamba, watoto walio na umri wa kati ya miaka mitatu na sita wamekuwa waathiriwa zaidi katika mwenendo unaoongezeka wa unyanyasaji wa kingono wa watoto unaotokana na wao wenyewe.
Wakfu ya Internet Watch ilisema kwamba, katika kipindi cha mwezi mmoja, wakfu hiyo iliiona mifano 51 ya picha za unyanyasaji wa watoto, hasa zinazotokana na wao wenyewe, hii ni ambapo watoto wanadanganywa kurekodi unyanyasaji wao wenyewe kabla ya kusambazwa mtandaoni hasa watoto walio na umri wa kati ya miaka mitatu na sita.
Aidha, zaidi ya nusu ya kesi hizi zilihusisha ndugu au rafiki wa mtoto.
“Watoto wadogo kama hao kufanyiwa unyanyasaji wa aina hii ni jambo linalojitokeza kwa sasa, maana si jambo ambalo tumeliona hapo awali na hii ni mara ya kwanza tunatoa takwimu za uhakika,” alisema Susie Hargreaves, mtendaji mkuu wa IWF. “Wachambuzi wetu wa mstari wa mbele, kwa sasa wanaona watoto wadogo na walio wachanga zaidi wakisogelewa, wakitunzwa na kulazimishwa na wanyanyasaji mtandaoni.”
IWF, ambayo huendesha simu ya dharura ya Uingereza pia inaripoti matukio ya nyenzo za unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto [CSAM] kote ulimwenguni, huku ikisema kuwa, maudhui yanayozalishwa yenyewe yanaundwa kwa kutumia kamera za wavuti au simu mahiri na kisha kusambazwa kwenye majukwaa kadhaa.
Ilisema kwamba, theluthi mbili ya ripoti hizo, ambazo zilisajiliwa kati ya Oktoba tarehe 11 na 10 Novemba mwaka jana, zilikuwa picha au video zilizonakiliwa, au zilikuwa na watoto ambao walionekana zaidi ya mara moja.
“Katika baadhi ya matukio, watoto wanafundishwa, na kulaghaiwa ili kutayarisha na kushiriki picha au video ya ngono yao wenyewe.
Picha hizo zinaundwa na watoto, na kwa mara nyingi katika vyumba vyao vya kulala au chumba kingine kilichopo katika mazingira ya nyumbani na hakuna mnyanyasaji aliyepo kimwili karibu nao, ila anaweza kuwepo kupitia mtandao,” ilisema IWF.
IWF ilisema kwamba, picha na video kadhaa zilionekana zikionyesha watoto wakitazama kwa makini ndani ya kamera, labda kusoma au kutazama kitu na kisha kukiiga, na pia muonekano huu wa kujichukua picha na video, haikuonekana kana kwamba ni mara yao ya kwanza, kwani yaashiria kwamba, watoto hawa wamefunzwa na kulaghaiwa kwa muda mrefu mno.
Mwaka wa 2021 ulikuwa mwaka mbaya zaidi kwa IWF kutokana na visa vya unyanyasaji wa watoto mitandaoni, kwani iliripoti URL 252,000 zenye picha au video za watoto hasa wale walio chini ya umri wa miaka 18 wakinyanyaswa kingono, ikilinganishwa na 153,000 mwaka uliopita .
Kati ya matukio 182,000 ya nyenzo za kujifanyia wenyewe, ripoti 148,000 ziliashiria watoto walio na umri wa miaka 11 hadi 13.
Mwandishi-Khadija Mbesa