By Khadija Mbesa
Uchunguzi wa unyanyasaji wa kijinsia katika Kanisa Katoliki la Ufaransa umegundua kuwa, watoto wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 300,000 walikuwa wahanga wa unyanyasaji mikononi mwa makasisi tangu 1950, Jean-March Sauve, mkuu wa tume iliyokusanya ripoti hiyo.
Kashfa kuu huko Ufaransa ni ya hivi karibuni ilikumba Kanisa Katoliki la Roma, ambalo limetikiswa na kashfa za unyanyasaji wa kijinsia kote ulimwenguni, mara nyingi zikiwashirikisha watoto, katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Tume ilianzishwa na maaskofu Wakatoliki huko Ufaransa mwishoni mwa mwaka wa 2018 ili kutoa mwanga juu ya dhuluma na kurudisha imani ya umma kwa Kanisa wakati wa kushuka kwa makutaniko.
Sauve alisema mbele ya hadhara, uwasilishaji wa ripoti hiyo kwa umma, kuwa shida bado ipo. Aliongeza kuwa , Kanisa limekua na zaidi ya miaka kumi tangu 2000 na bado linaonyesha kutowajali kabisa wahasiriwa.