Watoto Waliolelewa Katika Hali ya Mabadiliko ya Hewa

By Khadija Mbesa

Watoto na vijana waliong’olewa na kulelewa katika mazingira ya mabadiliko ya hali ya hewa, hubeba mzigo wa athari zake,
ila pia wanaweza kuwa mawakala muhimu wa mabadiliko haya.

Mabadiliko ya hali ya hewa tayari ni changamoto ya moja kwa moja kwa haki na ustawi wa watoto. Watoto bilioni moja, ambayo hii ni karibia nusu ya watoto duniani kote, wako katika ‘hatari kubwa’ ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa .Watoto hawa wanakabiliwa na mchanganyiko hatari wa kukabiliwa na majanga mengi ya hali ya hewa na ufikiaji mdogo wa huduma zinazowajengea uwezo wa kustahimili.

Hali ya hewa inabadilika kila mahali, na watoto na vijana waliotimuliwa kutoka katika makazi yao ya muda mrefu, kambi za wakimbizi, makazi duni ya mijini au miji mikubwa yenye shughuli nyingi, ni miongoni mwa walioathiriwa zaidi na athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Lakini watoto hawapaswi kuonekana kama watazamaji tu katika kukabiliana na changamoto zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa, ila watoto na vijana walioondolewa wanaweza pia kuwa mawakala muhimu wa mabadiliko. Wana ujuzi muhimu, uzoefu na mawazo tunayohitaji ili kukabiliana vyema na mabadiliko ya hali ya hewa na lazima wawe washirika katika kuunda ufumbuzi.

Madhumuni ya muhtasari huu ni kuibua mazungumzo juu ya uhusiano muhimu kati ya hali ya hewa, uhamaji na utoto pamoja na athari zake kwa sera na uwekezaji. Kwa kuangalia kile tunachojua, ambapo athari mbaya zaidi za mabadiliko ya hali ya hewa, udhaifu na migogoro huingiliana, na ambapo uhamaji wa watoto ni tokeo na mkakati wa kukabiliana, tunapata picha ya wazi zaidi ya jinsi uhamaji unaweza kutolewa ili kubadilisha changamoto hizi kuwa fursa amabyo itakuwa sambamba na watoto na vijana walioondolewa katika makazi yao.

“Mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa na uharibifu wa mazingira ni vita kwa ajili ya maisha yetu ya
baadaye. Ndio maana tunahitaji vijana kusimama kidete kupigania hali ya hewa katika miji yao,
majimbo na nchi… Pia tunaomba mataifa yaliyo na maendeleo, kufanya kazi pamoja ili kukaribisha zaidi
watu waliohamishwa na mazingira ndani ya mipaka yao, kuwapa usalama na
malazi. Hii ni ishara ya mshikamano wa kimataifa, wakati tunaona idadi kubwa ya watu, wanaondoka katika nchi zao kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na uharibifu wa mazingira.”

KIBIRITI MAJUTO, 23-YEAR-OLD, MKIMBIZI KUTOKA JAMHURI YA DEMOKRASIA YA KONGO(DRC)

Kati ya mwaka wa 2014 na 2018, watoto idadi 761,000 walikuwa wakimbizi wa ndani kutokana na dhoruba na mafuriko kote
katika kisiwa kidogo cha Karibea Kinachoendelea Mataifa (SIDS) hili ni ongezeko la mara sita ikilinganishwa na idadi ya 175,000 waliokimbia makazi yao kati ya mwaka 2009 na 2013.

Kumbuka, Migogoro ya hali ya hewa, ni migogoro ya haki za watoto.

Click to access

Children%20uprooted%20in%20a%20changing%20climate.pdf

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *