Watoto wa Wakimbizi wa Rohingya Kurudi Darasani

By Khadija Mbesa

Watoto wa wakimbizi wa Rohingya wamerudi darasani baada ya kufungwa kwa shule kwa mda mrefu zaidi ulimwenguni.

Zaidi ya watoto 164,000 wa Rohingya walio katika kambi za wakimbizi ya Cox’s Bazar nchini Bangladesh wamerejea katika vituo vya kujifunzia leo, baada ya usumbufu mrefu wa masuala ya kusoma ulimwenguni yaliyosababishwa na COVID-19.

Vituo vya kujifunzia vinavyoendeshwa na mashirika ya kibinadamu, ambayo hutoa elimu ya kiwango cha msingi kwa watoto wa wakimbizi wa Rohingya, ilifungwa miezi 18 iliyopita, na kuwaacha watoto wakiwa katika hatari ya ndoa za utotoni na ajira ya watoto kama njia ya kumudu mahitaji ya familia.

Serikali ilitangaza kuwa, vituo vya kujifunzia vinaweza kufunguliwa tena kwa watoto wa darasa la 2 hadi la nne baada ya kushuka kwa viwango vyema vya upimaji wa COVID-19 kitaifa na katika Cox’s Bazar iliyopungua kwa karibia asilimia tano wiki hii kutoka kwa asilimia zaidi ya 30 mapema Agosti. Shule za Bangladeshi zilifunguliwa mnamo Septemba tarehe 12, lakini watoto wa Rohingya walikuwa bado wanasubiri kuendelea na masomo yao.

Save the Children ilikaribisha kufunguliwa upya kwa vituo vya kujifunzia lakini pia, ilitoa wito kwa serikali kuwaruhusu vikundi vingine vya umri pia warudi kwenye madarasa yao.

Taslim, mwenye miaka 9, alisema itasaidia kwa walimu kutumia mtaala wa Myanmar na kuwa na walimu kutoka Myanmar.

“Hii itanisaidia kuwa daktari au mwalimu na kuweza kutimiza ndoto zangu,” aliiambia Save the Children.

Mkurugenzi wa Save the Children Nchini Bangladesh, Onno Van Manen, alisema kuwa, watoto na familia za Rohingya walikuwa na hamu ya kurudi kwenye masomo na elimu bora.

“Jitihada zinahitaji kurudiwa maradufu ili kutoa elimu bora kwa watoto wa Rohingya. Hii inaweza kupatikana kwa kupitia ufikiaji wa jamii na kushawishi familia zirudishe watoto wao shuleni na kuanza tena utoaji na upanuzi wa mpango wa majaribio ili kuwaruhusu watoto wa Rohingya kusoma kwa lugha yao ya mama kwa kutumia mtaala, “alisema.

Save the Children, kwa msaada wa waalimu wa Rohingya na Bangladeshi, wametoa elimu kwa wakimbizi wa Rohingya na jamii inayowakaribisha katika vituo 100 vya mafunzo katika kambi za Cox’s Bazar tangu mwaka 2017 wakati karibia wakimbizi milioni moja wa Rohingya walipokimbia Myanmar kwenda Bangladesh.

https://reliefweb.int/report/bangladesh/rohingya-refugee-children-back-classroom-after-one-world-s-longest-school-closures

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *