Watoto wa Mtaani na Umaskini

By Martha Chimilila.

Umaskini ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binadamu kama vile chakula, maji salama, huduma za afya, mavazi na nyumba, kutokana na kukosa uwezo wa kununua. Tafiti zilizotolewa na UNICEF zinaonyesha kuwa, nusu ya watoto duniani wanaishi katika hali ya ufukara ambayo ni sawa na bilioni 1.1. Utafiti wa ‘Makadirio ya Ulimwengu ya Watoto katika Umaskini wa Kifedha (2020)’ inaonyesha kuwa, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, theluthi mbili ya watoto wanaishi katika Kaya ambazo zinatumia chini ya dola 1.90 kwa siku. 

Umaskini ni moja ya sababu inayochangia ongezeko la watoto wa mtaani, kwa nchi ya Kenya na Tanzania. Watoto wengi hukimbia hali ngumu ya maisha katika familia zao. Watoto wanaoishi mtaani wako katika hatari kubwa ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia na kujiunga na makundi maovu. 

Shirika la Railway Children (Fight for Street Children), ambalo linafanya kazi nchini Kenya na Tanzania, pamoja na Taasisi mbalimbali katika kampeni za kupunguza watoto wa mtaani. Lengo la shirika hili ni kuwahimiza watoto wa mtaani kuzingatia njia mbadala za kimaisha. Wafanyakazi wa shirika hilo, wanafanya kazi usiku na mchana katika kutengeneza Mawasiliano na mahusiano mazuri ili kuweza kupata matokeo chanya. Changamoto wanazokumbana nazo moja wapo ni kupata taarifa sahihi za wazazi wa watoto hawa ili kuweza kufanya Mawasiliano nao.  

Katika kampeni ya kupunguza watoto wa mtaani, Shirika limefanikiwa kutoa ushauri nasaha, kuwarudisha nyumbani baadhi ya watoto na kuwaandikisha shule ili wapate elimu. Ushirikiano baina ya polisi na matumizi ya teknolojia kama Google Earth, umerahisisha kuwakutanisha watoto wengi na wazazi au walezi wao. Shirika hutoa fedha kwa familia ambazo zimekubali kuwapokea watoto hao ili kurekebisha hali ya uchumi wa Kaya. 

Nini kifanyike ili kupunguza Tatizo la Ongezeko la Watoto wa Mtaani: 

Ushirikiano wa jamii katika kazi za maendeleo, kama kuanzisha kwa michango mbalimbali ya kusaidia kaya maskini kama jamii ifanyavyo wakati mtu anapoamua kuoa au kuolewa au matatizo kama vifo. 

Ufuatiliaji wa sera za kimaendeleo, serikali inapaswa kuongeza nguvu katika utekelezaji wa sera za maendeleo ili kuweza kupunguza umaskini katika Kaya. Serikali katika Jangwa la Sahara zimetengeneza sera nyingi ambazo hamna ufatiliaji wa karibu. 

Kuanzisha vikundi na kutoa elimu za biashara, hii itasaidia kupunguza wimbi la umaskini katika ngazi ya familia. 

Source: https://www.railwaychildren.org.uk/what-we-do/our-work-in-east-africa/our-work-at-street-level-in-east-africa/ 

2 thoughts on “Watoto wa Mtaani na Umaskini”

  1. Shukrani Sana Kwa maelezo mazuri.

    Watoto WA mitaani wanaonekana kupuuzwa na wakati mwingine watu ama serikali inawajumhisha na kutoa sababu za pamoja WAO kuwa mitaani lakini ikumbukwe kuwa siyo Kila mtoto yupo mtaani Kama matokeo ya umasikini na ifike mahala jamii ama serikali itambue kuwa imekwisha kujenga Daraja kubwa Sana kati yao na hawa watoto ivyo siyo rahisi kupata takwimu sahihi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *