Wamlilie nani? Waelekee wapi?

By Khadija Mbesa

Asia imewapa Kisogo watoto wa Rohingya. Hakuna mtoto yeyote, anayepaswa kuishi na Hofu!.

Abul kijana mwenye umri wa miaka 16 ameishi maisha yake yote kwa hofu. Kama mtoto wa Rohingya kukulia katika Jimbo la Rakhine huko Myanmar, alikuwa akiteswa na kidhalilishwa mara kwa mara. Alishuhudia mamake na dadake wakipigwa.

Zaidi ya miezi 18 iliyopita, alipokuwa na umri wa miaka 15 tu, Abul aliiacha familia yake nyuma na kukimbilia Malaysia kwa matumaini ya kujenga maisha bora. Ila Malaysia haitambui Rohingya au watu wengine wanaokimbilia nchini kama wakimbizi, na kutokuwa na hati na kupigwa marufuku kwenda shule au kufanya kazi Abul anaishi kwa hofu ya kukamatwa wakati wowote.

“Tangu nilipofika, nimekuwa nikiogopa,” alisema. “Siendi nje ya nyumba ikiwa sihitaji kitu na naogopa kukamatwa na polisi.

Abul ana sababu nzuri ya kujawa na hofu kwani ndani ya wiki hii tu, vikundi vya haki za binadamu vililaani bango na idara ya uhamiaji ya Malaysia ambayo ilionyesha wakimbizi wa Rohingya kama tishio la usalama wa kitaifa . 

Huyu ni mtoto mmoja kati ya watoto kadhaa ambao wanapitia shida zizi hizi.

Ni hadithi ambayo inafahamika kwa mamia ya maelfu ya watoto wa Rohingya kote Asia, ambao wanalazimika kuishi pembezoni mwa jamii – hali ambayo haipaswi kuendelea. Kwa muda mrefu wanashindwa kurudi nyumbani kwao Myanmar, kwani usalama wao lazima ulindwe na mamlaka katika nchi walizokimbilia.

Kuna watoto 700,000 wa Warohingya Asia, na wengi wao wanaishi nje ya nchi yao, Myanmar. Kinachotambulika zaidi ni nusu milioni ya watoto wanaoishi katika kambi za wakimbizi huko Bangladesh, ambapo mamia ya maelfu ya watu wa Rohingya walikimbilia kutoka Myanmar ili kutoroka vurugu na jeshi la Myanmar mnamo 2017.

Hii ilikuwa tu sura ya hivi karibuni katika hadithi ndefu ya unyanyasaji: kwa miongo kadhaa, idadi kubwa ya Rohingya wametafuta kimbilio katika nchi zingine za Asia.

Ripoti mpya ya Save the Children inaangazia masaibu ya watoto wa Rohingya katika nchi tano kote Asia: Myanmar, Bangladesh, Malaysia, Thailand, na Indonesia. Watoto hawa wote wana kitu kimoja sawa: Popote walipo na kokote waendako, wanaishi pembezoni mwa jamii, wakiwa katika hatari ya kukamatwa, kudhalilishwa, na kunyonywa. 

Msichana mmoja wa miaka 11, ambaye mashua yake iliwasili Indonesia mnamo Septemba mwaka jana, alituambia: “Tulikuwa baharini kwa miezi. Nilihisi kiu lakini hakukuwa na maji ya kutosha. Hakukuwa na chakula. Sikuweza kusonga kwa sababu mashua ilikuwa ndogo sana. Nilikuwa na huzuni na nimechoka. ”

Watoto hawa walio katika uso wa ardhi wakihofia maisha yao ya mbele, wamekata Tamaa na Asia haiwapatii kipaumbele kabisa. Unyanyasaji wa kijinsia, kutopata Elimu, kuteswa na kupata vichapo vikali ndio mambo yaliokuwa utaratibu wa kila siku.

Jumuiya ya kimataifa lazima ijitolee na kutoa fedha kusaidia wakimbizi wa Rohingya kila mahali. Na serikali katika eneo hilo pia lina jukumu la kuhakikisha haki, usalama, utu, na ubinadamu wa watoto wa Rohingya wanaoishi ndani ya mipaka yao, kuhakikisha kuwa wanaweza kuishi na kustawi katika Jamii.

Source: https://thediplomat.com/2021/06/stranded-stateless-imprisoned-how-asia-is-failing-rohingya-children/

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *