Viwango vya Ndoa za Utotoni Vimeongezeka

17TH MAY 2022

Kulingana na data mpya iliyotolewa leo na Save the Children,Viwango vya ndoa za utotoni vimeongezeka kwa kiasi kikubwa miongoni mwa watoto waliolazimishwa na migogoro kuishi katika kambi, makazi yenye watu wengi zaidi katika eneo la Cabo Delgado Kaskazini mwa Msumbiji.

Kati ya Januari na Machi mwaka wa 2022, wakala ulirekodi kesi 108 za ndoa za utotoni katika wilaya ya Pemba, Metuge, Chiure, na Montepuez za Cabo Delgado, hii ikilinganishwa na kesi 65 kati ya Oktoba na Desemba mwaka jana.

Kati ya Januari na Machi, idadi ya watoto walioolewa hivi karibuni, iliongezeka polepole, kutoka kwa watoto 6 mnamo Januari, 32 mnamo Februari na 70 mnamo Machi.

Huu ukiwa mwaka wa tano wa mzozo huu maeneo ya Cabo Delgado ambao hauna matumaini ya kuwa na mwisho, Cabo Delgado imeonyesha athari mbaya kwa binadamu, ikiwemo utekaji nyara, ukataji wa vichwa, pamoja na udhalilishaji mwingi wa watoto.

Data kuhusu ndoa za utotoni inakuja kupitia mpango wa ulinzi wa watoto wa shirika la Save the Children ambao huwasaidia watoto wanaopitia hatari kubwa hasa katika masuala ya afya na ustawi wao, hii ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni na pia kutelekezwa na masuala ya afya ya akili. Advertisementshttps://c0.pubmine.com/sf/0.0.3/html/safeframe.htmlREPORT THIS AD

Ongezeko la wasiwasi la ndoa za utotoni ni matokeo baada ya mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na dhiki ambazo familia nyingi zimekuwa zikikabiliana nazo ndiposa waweze kuishi katika vituo vya usafiri au changamoto za kuanza maisha mapya katika maeneo mapya. 

Wazazi wengi wanakabiliwa na chaguo baya la kushindwa kulisha familia zao au kuwapa nyumba watoto wao wote, na badala yake inawalazimu kuwaacha waoe au waolewe ili wapunguze mzigo kwenye familia.

Tangu mwaka wa 2017, migogoro katika jimbo la Cabo Delgado imesababisha watu 784, 564 kuhama makazi yao , wakiwemo watoto 370,000. 

Mgogoro huo umewaacha watu milioni 1.5 wakiwa na mahitaji kadha wa kadha , na kuna ripoti zinazoendelea za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na za watoto, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara, kuandikishwa na kutumiwa kwa watoto katika makundi yenye silaha.

Kwa kuzingatia hali halisi ya mgogoro na mazingira magumu ya hali ya hewa ya mkoa na nchi, Shirika la Save the Children limejiandaa ipasavyo ili kusaidia katika mikoa na wilaya ambazo zinaweza kuhusishwa katika mgogoro au kuathiriwa hivi karibuni.

Mwandishi-Khadija Mbesa

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *