Vita vya Syria

By Martha Chimilila

Jitihada za Belgiji katika Kumlinda Mtoto dhidi ya vita ya Syria

Ubelgiji ni nchi ya kwanza katika bara la Ulaya, kufanya maamuzi ya kuwachukua mama na watoto kutoka kambi za Jihadi za Syria. Mamia ya Wazungu katika bara la Ulaya, walisafiri kwenda Syria kujiunga na Islamic State, takribani asilimia 40 ni watoto na wanawake. Wazungu hao walinaswa katika kambi zinazoendeshwa na Wakurdi kaskazini mwa Syria.

Nchi nyingi za Ulaya haziruhusu wananchi waliosafiri kwenda Syria kurudi, lakini Ubelgiji ilitangaza harakati za kuwarudisha mama na watoto.

Waziri Mkuu Alexander de Croo alitangaza jitahada hizo mnamo machi ya kuwa Ubelgiji itafanya kila njia kuwarejesha wale wote walio katika kambi zilizo na watu chini ya miaka 12, akisema hii italeta ustawi wa kijamii na maadili, pia kusaidia kupunguza ongezeko la magaidi”

Ripoti zinasema mara tu watakaporejeshwa kutoka kambi ya Jihadi (Roj), kaskazini mwa Syria, wamama hao watakamatwa na kushtakiwa, na maafisa wa kupambana na magaidi, wakati watoto watapatiwa matunzo katika sehemu maalumu.

“Heidi De Pauw, Mkurugenzi wa asasi ya kiraia inayojulikana kwa jina la (child focus) Mtazamo wa Mtoto, alisifu uamuzi uliotolewa na Waziri Mkuu. Aliongea na shirika la habari la AFP, kuwa watoto wanapaswa kupewa matunzo na ulinzi dhidi ya maeneo yenye vita”

Taarifa hii imechapishwa na ‘BBC Habari’ siku mbili zilizopita.

Source: https://www.bbc.com/news/world-europe-57870808

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *