Uzito wa Ukiukwaji wa Haki za Watoto Kaskazini mwa Ethiopia

By Khadija Mbesa

Kama walivyosema, Fahali wawili wakipigana basi manyasi ndio huumia. Miezi kadhaa baada ya vita vya ndani huko kaskazini mwa Ethiopia, kumekua na vifo vya maelfu ya watu, mamilioni ya wakimbizi, na kusababisha mashtaka ya ukatili kama utakaso wa kikabila, serikali ya Ethiopia na washirika wake hawajaonyesha dalili yoyote ya kurudisha vikosi vya jeshi kutoka mkoa wa Tigray, hili likikusudia unyanyasaji na unyonyaji wa Watoto na kutengana kwa wazazi na Watoto wao baada ya mzozo huo.

UNICEF ikiongelea kuhusu swala hili ikisema kuwa,

“Zaidi ya watoto 6,000 waliojitenga wametambuliwa na kusajiliwa kwa ulinzi na usaidizi. Tunaogopa kuna watoto wengi zaidi ambao wanahitaji msaada katika maeneo ambayo hatuwezi kufikia kwa sababu ya ukosefu wa usalama au vizuizi vya ufikiaji vilivyowekwa na washiriki wa mzozo. Ufuatiliaji na kuungana kwa familia kunazuiliwa hili kuchachia mawasiliano machache, uwepo mdogo wa wafanyikazi wa kijamii, na ufikiaji mdogo kwenye mistari ya udhibiti.

“Wanawake na wasichana bado wanakabiliwa na vitendo vya kutisha vya unyanyasaji wa kijinsia. Zaidi ya manusura 540 wamepata msaada kupitia programu za UNICEF tangia  kuzuka kwa mapigano mnamo Novemba 2020, lakini kuna ukosefu wa usalama kwa jumla, na hofu ya kulipiza kisasi, hili huacha idadi isiyojulikana ikishindwa kupata huduma zinazohitajiwa kwa haraka.

“Watoto, wazazi na walezi huripoti wasiwasi mkubwa na shida, wakisema kuwa wanahofia kulipizwa kisasi au kushambuliwa. Wavulana  wanazungumza juu ya hofu ya kuajiriwa na kutumiwa na wahusika kwenye mzozo huo. Washirika wa UNICEF wanaendelea kuripoti kukamatwa kwa Watoto hao na kuwekwa kizuizini kiholela .

“Watoto ndio wanaumia katika mzozo huu. UNICEF inatoa mwito kwa pande zote kuheshimu wajibu wao wa kimsingi wa kuwezesha ufikiaji bila vikwazo na endelevu kwa raia wanaohitaji msaada, haswa kwa watoto. Zaidi ya yote, tunatoa wito kwa wahusika wote kufanya kila kitu ndani ya uwezo wao kulinda watoto dhidi ya unyanyasaji, unyonyaji , na kuzuia kutenganishwa na wazazi wao au walezi kwa msingi. “

source; https://www.unicef.org/press-releases/children-northern-ethiopia-dire-need-protection-and-assistance

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *