Uzinduzi wa Ripoti ya Kimataifa ya UNICEF kuhusu Watoto wenye Ulemavu

By Khadija Mbesa

Kwa mara ya kwanza, UNICEF hapo leo, imezindua ripoti ya takwimu za watoto wenye ulemavu kimataifa.

UNICEF Inajiunga nanyi nyote, ili kujenga ulimwengu ambapo watoto wenye ulemavu waweze kufikia uwezo kamili, Kukua na afya, kuelimika, kulindwa na kushirikishwa katika jamii zao.
Hiki ndicho kitovu cha dhamira yetu, kutambua haki za kila mtoto na kushughulikia suala la kutoonekana kwa watoto wenye ulemavu na kukuza ushiriki wao kamili ni hatua muhimu katika kuimarisha haki zao.

Ni lazima waonekane madarasani, mitaani, kwenye vyombo vya habari na katika sera na sheria za umma, La muhimu zaidi, sauti zao lazima ziwe kiini cha uamuzi wowote unaohusu maisha yao.Haki za watoto wenye ulemavu, zimefafanuliwa wazi mwaka wa 2006 katika haki za kawaida za watu wenye ulemavu ambazo zimeidhinishwa na zaidi ya nchi 180.

NAIBU MKURUGENZI MTENDAJI, BW OMAR ABDI

Takwimu hizi zimetoa msingi maalum wa kuelewa watoto hawa ni kina nani na upeo wa kuendelea.

Mkakati huu, wa sera ya ulemavu, unatarajiwa kuongoza kazi kuhusu ulemavu, na ushirikishwaji wa muongo ujao na zaidi.

Kila mtoto ana haki ya ulinzi na kupata masomo shuleni, kwani watoto wengi walemavu wananyimwa haki ya kuingia darasani ili kuweza kusoma na wenzao.

Takwimu hizi zitakuwa na jukumu muhimu katika kuongoza kazi yeyote ile, kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wao, na ubora wa data ni wajibu wa pamoja katika kujitolea kufanya kazi na serikali na mashirika ya kiraia yenye nguvu na Mifumo ya Kitaifa ya Data huku ikikuza ujuzi na uwezo wa kuzalisha uchambuzi muhimu wa maarifa.

Data ni hitaji la msingi, na zaidi ya hayo, ugawaji wa rasilimali na bajeti kwa watoto wenye ulemavu hauwezekani bila data.

SULEYMAN ARSHAD-PAKISTAN

Ukosefu wa data juu ya watu wenye ulemavu wakiwemo watoto, ina maana kwamba wahusika katika nafasi ya ulemavu hawawezi kuendeleza sera za ulemavu, kujumuisha ulemavu katika utayarishaji wa programu au kwa ufanisi katika programu mpya za watu wenye ulemavu.

Bila upangaji mzuri wa programu, watoto wenye ulemavu wanaachwa katika mazingira magumu kwani vyanzo vya udhaifu havijashughulikiwa vyema

KIBE YOHANA-KENYA

Data husaidia kuondoa vikwazo ambavyo watoto hawa hukabiliana navyo katika elimu ya afya na nafasi ya jamii

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *