Uzinduzi wa Kilabu 4-K

By Khadija Mbesa

Kuungana, Kufanya na Kusaidia Kenya, kilabu inayozinduliwa upya na wizara ya kilimo na teknolojia  pamoja na Mheshimiwa Rais Uhuru Muigai.

Uzinduzi wa Kilabu 4-k ambao umefanyika Ijumaa ya leo tarehe 4 mwezi wa 6 mwaka wa 2021.

Wanafunzi kutoka shule mbali mbali walileta miradi yao ya kilimo kati ya shukle hizo ni, shule ya wanaume ya Mvuti walikuwa na mradi wa Ufugaji wa Samaki katika maeneno ya Ukame.

Shule ya Katheka kai, ambao walitufunza Bustani ya Mboga jongevu, wametumia rasilimali zilizopo nchini ili kuunda bustani ambayo ni rahisi hasa kwa watu katika maeneo ya mjini.

Shule ya Upili ya wasichana ya Ruthimitu ambayo ilituonyesha aina mbalimbali za mimea na matumizi yake.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhe. Anne Nyaga aliainisha masuala ambayo yalikuwa changamoto kwa vijana katika kushiriki sekta ya Kilimo tangu mwaka 2016, miongoni mwao ni, fedha zisizoridhisha, kukosa maarifa, taarifa na ujuzi, mwendo wa kufufua na kuitengeneza upya klabu ya 4k inarahisisha mambo mengi na inawezesha maendeleo na maslahi ya mtoto katika shule ya upili.

Jemima Kanini Mbogo kutoka Shule ya Msingi ya Scholastica Catholic akimpa shukrani Mheshimiwa Uhuru Muigai “Mheshimiwa, kwa niaba ya Wanachama wa klabu ya 4 -k na watoto wote, nafurahi kuwashukuru kwa dhati, Kwa Kuzindua na kuunda upya Mpango wa kilabu hii, mpango ambao utatunufaisha sana sisi watoto,”

Vijana kutoka pande mbali mbali za Kenya wamempa pongezi Bwana Rais Uhuru Kenyatta na kutoa shukran abadan kwa kuzindulia tena kilabu ya 4-k.

Rais Uhuru Kenyatta, “Kwa pamoja tunazindua na kuitengeneza tena klabu hii ya 4k, mpango wa kuendeleza vipaji vya vijana wetu na kuwatia moyo, harakati za klabu 4k zimekuwa kitambaa cha taifa letu kutokana na mchango wa jamhuri yetu, ninaamini kwamba kilimo kina uwezo wa kutoa fursa zaidi za ajira na pia kujiajiri.

“Kupitia Mkakati wa Vijana wa Biashara ya Kilimo Kenya 2018-2022, Tunatambua Changamoto ikiwa ni pamoja na mitazamo hasi ya biashara ya kilimo, Tunapozingatia vikwazo hivi, lazima tujikite sawa katika kujenga na kuwatayarisha Vijana katika biashara ya kilimo kutoka shule ya msingi, hii itahitaji ushirikiano wa wamiliki wa vigingi na serikali zetu za kaunti”

Rais Uhuru Muigai ameahidi kwamba hii haitakuwa awamu ya pekee, bali kutakuwa na nyingi Zaidi zitakazokuja mbeleni.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *