Ustawi wa Afya ya Watoto baada ya Janga la Uviko 19

By Martha Chimilila

Ustawi wa afya ya watoto kulingana na ufafanuzi uliotolewa na Shirika la kusimamia haki za watoto duniani UNICEF: ni uwezo wa nchi na familia au jamii kusimamia ukuaji wa afya, upatikanaji wa elimu, kulinda na kusimamia haki za watoto kama hisia za kupendwa, kuthaminiwa na kujumuishwa katika familia au jamii zinazowazunguka. UNICEF inachukua njia ya kiikolojia kama njia ya kupima ukuaji wa ustawi wa afya ya mtoto, inayojumuisha maisha ya mtoto kwa ujumla.

Mwanzoni mwa mwaka 2020, dunia ilikumbwa na Janga la Uviko 19 na kusababisha kutolewa kwa miongozo mbalimbali na shirika la Afya duniani. Miongozo hii ilidhamiria kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa, lakini miongozi hii imeleta athari kubwa kwa afya ya watoto na ustawi wao kwa ujumla. Idara za dharura za watoto zilibadilisha mfumo wa utoaji wa huduma ili kukabiliana na janga hili.

Janga la Uviko-19 limeleta athari za kisaikolojia kwa watoto, athari zimeonekana kwa ngazi ya familia, mtoto na hata jamii na hii ilisababishwa na matamko ya nchi mbalimbali kwa kufunga shule, sehemu za michezo na kupunguza mikusanyiko. Wataalamu wa afya ya watoto walisema hii imesababisha kuongezeka kwa tatizo la afya ya akili kwa watoto.

Mabadiliko ya shughuli za kielimu, kijamii na burudani ziliondolewa kwa watoto na kupunguza mfumo wa mwingiliano wa kijamii. Mtoto ili aweze kukua vyema inapaswa kushiriki katika michezo mbalimbali, pia kubadilisha mazingira yanazomzunguka. Kwa kufanya hivyo kuna chochea ukuaji wa ubongo na afya kwa ujumla. Lakini katika kipindi hiki dunia ikiwa inapambana na Janga la Uviko 19 hali imekuwa tofauti, maana watoto waliacha kuishi maisha yao ya kitoto”

Vizuizi vilivyoletwa na Janga la Uviko 19 katika sekta ya afya vimeleta athari kubwa kwa afya na ustawi wa watoto kisaikolojia. Athari ni mbaya zaidi kwa watoto wenye ulemavu na magonjwa sugu. Nchi nyingi za Afrika zimeonyesha mapungufu makubwa za rasimali katika kupunguza au kudhibiti tatizo hiliMmoja wa wataalamu wa afya alitoa ushauri na kusema;

“Katika kipindi ambacho bado tunapambana na Janga hili, watunga sera na watoa huduma lazima wahakikishe kwamba, wanatoa huduma rafiki hasa kwa watoto na kuwatia moyo ili kupunguza tatizo la ustawi wa afya kwa watoto”

Source; https://bmchealthservres.biomedcentral.com/articles/10.1186/s12913-021-06284-9

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *