Usalama wa Watoto Wetu

By Khadija Mbesa

Visa vingi vya utekaji nyara vimekuwa vikitokea pande nyingi za Kenya, huku watoto wakiwa waathiriwa zaidi, je Watoto wetu wako na usalama? hili ndilo swali kuu linalopitia akili ya kila mzazi.

Watoto hawako salama, si shuleni wala nyumbani.

Hivi karibuni, Shantel Nzembi wa miaka minane alipotea kutoka nyumbani kwao Kitengela wakati alikuwa ametoka kwenda kucheza na Watoto wanzake.

Baada ya masaa kadhaa, mamake alipokea simu kutoka kwa watu wasiojulikana ambao walidai kuwa, Shantel yupo mikononi mwao huku wakidai fidia.

Siku chache baadaye, mwili wake ulipatikana umetupwa Orata huko Noonkopir akiwa ashaaga dunia.

Vivyo hivyo Daraja la Moi lililo Eldoret, mwili wa mschana mwenye umri wa miaka 13 ulipatikana na wanakijiji.

Linda Cherono, aliyekuwa ametoka kwa jamaa zake huku akiaga anaenda saluni mjini, alitekwa nyara na hiyo ndiyo ilikua mara ya mwisho ya kuonekana kwake. Msichana aliyekuwa na asili ya Baringo, alikua ameenda matembezi Eldoret kwa jamaa zake huku akingoja kuingia kidato cha kwanza mnamo Agosti.

Picha za CCTV kutoka duka la karibu zilionyesha Cherono akitembea nyuma ya mgeni ambaye polisi wanamshuku kama muuaji.

Ndoto na maono ya roho hizi mbili zilifupishwa na mikono ya kifo ya ukatili iliyowekwa juu yao na watu wabaya.

Hizi ni kesi mbili tu lakini jinsi jamii imegeuka kuwa mbaya, kuna wasiwasi mkubwa kwa Watoto wetu.

Majumbani mwetu tu kuna wanafamilia wanaoweza kuwageukia Watoto wetu na kuwanyanyasa na kuwateka nyara hata huenda kuwakatiza Maisha yao.

hivyo ni visa vichache tu kati ya vingi, kila wiki kuna mtoto anayetekwa nyara kwa sababu ya fidia.

Hili ni jambo la kusikitisha mno, tutafanya nini ili tuweze kulinda Watoto hawa?

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *