Usafirishaji Haramu wa Watoto

By Martha Chimilila

Usafirishaji haramu wa watoto ni kitendo cha kuwaondoa watoto katika mazingira salama na kuwatumikisha katika biashara za unyonyaji au biashara ya ngono. Tanzania ni moja ya nchi ambayo iko katika mapambano dhidi ya vitendo vya usafirishaji haramu wa watoto. Katika mkoa wa Mbeya, Jeshi la polisi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuwatorosha na kuwauza watoto 13 wenye umri wa miaka 10. Watu hawa walifanya hayo, sababu walipata wateja katika nyumba za watu na kuchunga mifugo katika wilaya ya Mbarali. 

Bwana Urlich Mtei, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya aliongea na mwandishi wa gazeti la Mwananchi tarehe 7 September 2021, alisema kuwa: 

“Nimewakamata watu watatu kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji haramu wa watoto baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema. Tumewahoji na wamekiri kushiriki katika biashara ya usafirishaji haramu wa watoto kwa ujira wa shillingi elfu 20,000 kama atawafikisha sehemu wanapohitajika” 

“Tumebaini kuwa licha ya watuhumiwa hao kuwatorosha watoto, lakini kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakikubali pasipo kujua ni kinyume cha sheria na kuminya uhuru wao wa kupata elimu na makuzi katika familia “ 

“Tunaendelea na uchunguzi pamoja na kurejesha watoto kwenye familia zao. Kitendo cha kusafirisha binadamu ni kinyume cha sheria za nchi hivyo watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika” 

“Jeshi la Polisi halitovumilia uvunjwaji wa sheria kwa kuwa watoto hao bado wadogo na kitendo cha kutumikishwa kazi majumbani na kuhudumia mifugo ni kinyume cha sheria. Jeshi limeamua kutoa elimu bure hivyo mzazi yoyote atakayeendekeza tamaa na kumzuia mtoto wake asisome ni lazima atawajibishwa kwa mujibu wa sheria” 

Source: https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/mbaroni-kwa-kuuza-watoto-kwa-sh20-000-3542868 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *