Unyanyasaji wa kijinsia na mwanafamilia

By; Khadija Mbesa

Wakati mwingi Watoto wananyanyaswa kijinsi na watu walio karibu nao na sio wa mbali. Sote tumeona na tumeskia venye Watoto wananyanyaswa kijinsia na wajomba zao au baba zao wa kambo, wengine hata hua wananyanyaswa na baba yao mzazi. Mara nyingi unapata mtoto wa kike ndiye mwenye kuwa mhasiriwa katika mambo haya.

Swali ni, utajuaje unanyanyaswa kijinsia na mwanafamilia? Kwa maana Watoto wako na roho safi na isiyo na hatia basi wanaeza dhani ni mapenzi ya kifamilia tu bila maana ya ndani.

“Jambo la kwanza ni ukaribu wa mtoto na huyo mnyanyasaji, unaweza pata mtu huyo anakupatia zawadi mara kwa mara bila kuwa na tukio lolote, huku akikwambia venye atakupatia chochote unachotaka. Basi mtoto huwa anafurahia mno na anazidi kuwa na ukaribu Zaidi na mnyanyasaji huyo.

La pili ni wataanza kuwa sikio lako ukiwa na matatizo na wazazi wako, ama shuleni ama hata marafiki zako. Utaona kuwa anakupatia chenye huezi pata kwengine, UMAKINI, atakuskiza na kukupatia bega huku akikuambia venye uko mzuri, atafanya bidii ucheke ili usiwe na hasira. Wewe huna Habari ila anakuvuta kwa shimo lake polepole tu.

Atataka kuwa na uwepo wako kisirisiri huku akianza kukwambia usimwambie mzazi wako kuwa mmeenda mahali flani ama mmefanya nini. Anakufanya uwe na umbali na wazazi wako. Na wewe utaona mapenzi hayo unapata ni ya kifamilia tu na hayawezi kukuathiri kivyovyote.

Mwisho ataanza kukushika na kukugusa kusikofaa, huku akikwambia venye uko mrembo na venye unavutia, akikuuliza kama bado umepata mpenzi ama Rafiki wa kiume, kwani uko umri ambao mwili wako unaanza kuwa na mabadiliko. Hapo ndipo utaanza kuwa na wasiwasi na kutoka na raha kabisa kutokana na venye anakugusa. Utajaribu kumwambia hutaki hivyo lakini ataanza kukwambia ni kawaida kwa wanafimilia kuwa na uhuru wa kugusana ama kushikana hivyo.

Utaanza kuwa na uoga, hujui umwambie mzazi wako ama unyamaze, utaanza kujenga mafikira akilini mwako ukidhani wazazi wako watakulaumu wewe, unaanza kujiweka kwa umbali na mnyanyasaji huyo lakini bado unahisi vibaya. Mwisho utaamua kumwambia mzazi wako lakini bado hutaweza kuishi kama zamani kwani umenyanyaswa kijinsia na isitoshe na mwanafamilia, utaanza kuwa na masuala ya uaminifu. Utajifungia mbali na dunia huku ukidhani kuwa Maisha yako hayana maana kabisa.

Amka uone mwangaza, wewe ulikua mhasiriwa na hukuwa na makosa yoyote kwa lilokutokea. Jifunze jinsi ya kuishi na kuamini watu, haswa wazazi wako. Fungua moyo kwa wazazi ama kwa Rafiki yako wa karibu.”

Watoto wengi sana wananyanyaswa kijinsi na wanafamilia. Wazazi wanafaa kuwa na ukaribu na Watoto wao, ongea na wao mara kwa mara waonyeshe kuwa wanaweza jifunguka kwako. Wafunze maana ya familia na pia wafundishe jinsi ya kujikinga na unyanyasaji huo. Wasimwamini mtu yoyote na mwili wao.

follow us on

Twitter:https://twitter.com/mtotonews

subscribe to our YouTube channel:https://YouTube.com/mtotonewstv

Mtoto News is a Digital Online platform of news, information and resources that aims at making significant changes in the lives of children by making them visible. Read mtotonews.com or follow us on Twitter and Facebook@mtotonewsblog

1 thought on “Unyanyasaji wa kijinsia na mwanafamilia”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *