Umaskini na Tamaa yazika ndoto ya kuwa Mwalimu

By Martha Chimilila

Upendo John ni binti wa miaka 16, anayeishi wilaya ya Geita nchini Tanzania. Upendo alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi bora kitaaluma na mhitimu wa darasa la saba 2021. Kwa sasa Upendo ana mimba ya miezi miwili na amefukuzwa shule, hivyo hawezi tena kufanya mitihani ya kuhitimu darasa la saba.

Nini kilisababisha kujihusisha na mahusiano?

Upendo alisema hali ngumu ya maisha kwenye familia ndiyo iliyosababisha kuingia katika ushawishi, baada ya Kijana (Masumbuko) mjasiriamali kuahidi kumsaidia kwa mahitaji madogo madogo ya shule na binafsi.” Aliniahidi kuninunulia daftari na nguo za ndani, kwani nilikuwa na nguo ya ndani moja tu”. Upendo alisimulia yafuatayo:

Nilianza urafiki na Masumbuko John mwishoni mwa mwaka Jana na Januari mwaka huu, alininunulia madaftari (conte book) kwa ajili ya kuanza darasa la saba pamoja na nguo za ndani, kwa kulipa fadhila nilikubali kulala naye”

“Nilikubali kuwa rafiki yake ili niwe na nguo za ndani kama marafiki zangu”

Urafiki uliendelea kati yangu na Masumbuko, alininunulia nguo za shule na vitu vingine mbalimbali.

Aliponinunulia nguo za shule nilifurahi sana, maana nilikuwa natia aibu miongoni mwa wasichana waliokua na mavazi chakavu na mimi ni mmoja wapo. Hii ilikua ni mwezi wa tatu nikamshukuru tena na hapo ndipo nilipata mimba

Upendo anaongeza kwa kusema yafuatayo” Natamani muda urudi nyuma, nifanye maamuzi tofauti na niliyoyafanya”

Mwalimu Gerald Mkoloni, anakiri kuwa na changamoto ya utoro na mimba za utotoni katika kijiji cha Nkome. Mwalimu Gerald alisema yafuatayo” Sababu zinazochangia utoro na mimba za utoto ni wazazi kushindwa kufatilia mienendo ya watoto wao na kuwaacha kujilea wenyewe, huku wao wakihamia visiwani kwa shughuli za uvuvi

Uelewa mdogo wa jamii juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto, hasa watoto wa kike

Bi Edith Mpenzile, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita alisema ‘Kutokana na changamoto za mimba tumeanza kutoa elimu za afya ya uzazi kwa watoto wa kike, kujitambua, makuzi na Mabadiliko ya kimaumbile’

Bi Paulina Alex, Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za watoto, kina mama na haki za binadamu (NELICO) alisema yafuatayo “Hali ya mimba kwa watoto katika wilaya ya Geita ni mbaya na tunajukumu la kuliongelea tatizo hili na sio serikali peke yake

Source: https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/hongo-ya-sh2-000-ilivyopeperusha-ndoto-ya-kuwa-mwanajeshi-3486476

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *