By; Khadija Mbesa
Takriban Watoto 250 wamelazimika kukuzwa gerezani baada ya wazazi wao kuanza kutumikia kifungo wakiwa wana uja uzito.
Watoto hao walio na umri wa chini ya miaka minne wamekuwa wahasiriwa wa suala hili na kulazimika kutumikia kifungo cha wazazi wao huku wakiishi gerezani Pamoja na mama zao waliofungwa ili kuto
Watoto hao hushuhudia changamoto nyingi hapo gerezani ikiwemo kutopata lishe bora, kwani wanakula mlo ule ule wanaokula wazazi wao. Hili huchangia utapiamlo kwa Watoto. Si hilo tu bali wanapata upungufu wa pampers huku wakipewa moja tu kwa siku.
Watoto hawa watakuwa wakijua Maisha ya gerezani kwanza, jambo ambalo litachangia pakubwa katika ukubwa wake.
Baadhi ya wanawake wanaanza kutumikia kifungo wakiwa na Watoto wao na wengine huenda gerezani wakiwa wana uja uzito.
Kuna takriban Watoto 250 nchini Kenya ambao wako katika mfumo wa adhabu gerezani kwa sababu ya wazazi wao wa kike. Watoto hao wako katika magereza ya wanawake ambayo ni 43, kumi kati ya magereza hayo ndiyo yako na vituo vya kulea Watoto hii ikimaanisha asilimia sabiini na tano inahitaji usaidizi.
Kati ya mapendekezo ya kisheria ni, kuimarisha sheria zinazohusu Watoto walio katika mfumo wa adhabu gerezani, kubuni afisi ya Watoto itakayosughulikia kumrudisha katika jamii, upungufu wa umri wa Watoto kuishi gerezani, hukumu isiyo na hukumu ya ulezi na kutengeza miundo msingi bora ya kurudisha mama na mzazi katika jamii.