Ukeketaji Kuvushwa Mipaka

by Martha Chimilila

Unyanyasaji wa kijinsia ni tendo lenye kuleta madhara kwa mtu kulingana na jinsi yake. Hii inatokana na ukosefu wa usawa wa kijinsia, matumizi mabaya ya tamaduni na Kanuni za kimila. Takwimu zaonyesha kuwa,Tanzania ina asilimia 40 ya watoto wa kike walio chini ya miaka 15 waliofanyiwa unyanyasaji wa kimwili. Na takribani asilimia 17 wamefanyiwa unyanyasaji wa kijinsia katika Maisha yao. Jamii inatambua athari ambazo unyanyasaji wa kijinsia unaleta kwa kudhoofisha afya ya akili, ustawi wa Maisha ya wasichana na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wanaharakati mbalimbali duniani na asasi za kiraia kama ‘UNICEF na UNFP’ wapo katika mapambano ya kupinga ukeketaji kwa watoto wa kike. Tafiti zaonyesha kuongezeka kwa vitendo vya ukeketaji wa watoto kwa maeneo ya mipakani. Hii inatokea pale wasichana wanaoishi katika nchi ambayo mila hii inapingwa na sheria kali, wakeketaji wanavusha watoto kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine, ambayo sheria za nchi hazimbani mkeketaji.

Ukeketaji wa kuvusha mipaka unaoneka kukomaa Afrika ya Mashariki, katika nchi za Ethiopia, Kenya, Tanzania na Uganda. Hii inatokana na kwamba nchi hizi zimepakana na kuna mwingiliano wa tamaduni na mila. Makabila kama maasai, kurya ni moja ya makabila yanayopatikana katika nchi za Tanzania na Kenya. Hii inatokea hata kwa watoto walio chini ya umri wa mwaka mmoja.

Tafiti na thathimini zilizofanywa na UNFP katika nchi tano, zinaonesha ukeketaji hufanya kazi kama Kanuni ya kijamii. Sheria za nchi hizi tano ni tofauti na mkeketaji hawezi hukumiwa kwa kitendo alichokifanya katika nchi nyingine. Kutokana na utofauti wa sheria, umesababisha ongezeko kubwa la ukeketaji wa kuvuka mipaka na sheria haina uwezo wa kuwaadhibu.

Mambo yanayochangia ongezeko la Ukeketaji wa kuvuka mipaka;

Mila za pamoja, haswa kuoana hiyo imechangia vitendo vya ukeketaji. Hofu ya kukamatwa katika nchi ya asili na utofauti wa sheria katika nchi Jirani. Uwezekano na upatikanaji wa huduma za ukeketaji katika nchi Jirani. Vyanzo vya mapato kwa watahiri vinatoa moyo wa kuendelea na vitendo vya ukeketaji. Kutokuwepo kwa njia na sheria kali za ufatiliaji na kuripoti.

Nini kifanyike kupunguza tatizo la ukeketaji wa kuvusha mipaka?

  • Kuwekeza katika afya ya watoto wa kike na wanawake, elimu na uwezashaji kama vigezo muhimu na endelevu katika ukuaji wa uchumi na kijamii ili kuweza kuondoa tatizo la ukeketaji na kupata haki zao za msingi.
  • Kukemea ukeketaji wa matibabu, ambapo ukeketaji hufanywa na jamii yoyote ya mtoa huduma ya afya, iwe kwa umma au kliniki, nyumbani au mahali pengine.
  • Kuimarisha mifumo ya kisheria, sera na utekelezaji wa sheria juu ya ukeketaji kwa watoto.
  • Kushirikiana na wanaume katika jamii na Kupitia kwa pamoja mipango ya kupinga tatizo la ukeketaji, kwa kutumia njia mbadala na shirikishi kama viongozi wa jadi au Mashirika ya dini.
  • Kushirikisha vyombo vya habari kama redio na mitandao ya kijamii katika kutangaza ujumbe kuhusu athari za ukeketaji kwa watoto wa kike.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *