Uhaba wa Mvua na Ukame, Wawalazimu Watoto Kulazimishiwa Ndoa za Mapema

Khadija Mbesa

Watoto wa shule wanakabiliana na ukame unaokumba maeneo ya Pwani.

Wadau wa elimu na wanakijiji, waliripoti hapo jana kuhusu kuongezeka kwa visa vya kuacha shule na ndoa za kulazimishwa katika kaunti ya Kilifi na Tana River. Huku hayo yakijiri, wavulana katika maeneo mengine ya kaunti ya Kilifi, Kwale na Tana River wameacha shule ili kuchoma makaa na kuuza ili waweze kununua chakula cha familia zao.

Mbali na shughuli za kibiashara, wasichana wadogo na wavulana wamelazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji. Hapo jana, Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti ya Tana River, James Nyagah alisema kwamba, zaidi ya wasichana 25 wameolewa ili familia zao zipate mlo.

Changamoto za kupata elimu katika kaunti ya Kilifi na Tana River zinajulikana sana, lakini Nyagah alisema kuwa, ukame mkali umezidisha hali hiyo. Katika maeneo ya mbali ya kaunti hiyo, kuna ripoti ambazo hazijathibitishwa za wasichana kulazimishwa kuolewa ili familia hizo zipate mahari ya kununua chakula. “Zaidi ya wasichana 25 wameolewa ili familia ipate chakula,” alisema Nyagah.

Katika eneo la Magarini kaunti ya Kilifi, wavulana wengi wameacha shule ili kuchoma makaa, angalau ili kuendeleza familia zao.

Kulingana na Dama Katana, mkazi wa Ganze, wasichana wanaokwenda shule wakati mwingine wanalazimika kusalia nyumbani wakati wa hedhi kwa sababu ya ukosefu wa maji ya kuoga.

 “Wasichana wengi hubaki nyumbani kwa sababu wanakosa maji ya kuoga vizuri na kufua nguo zao wakati wa hedhi,” alisema.

Chama cha Msalaba Mwekundu cha Kenya kinakadiria kuwa, watu 145,000 huko Kilifi wanatatizika kunusurika na hali ya njaa. Idadi hiyo inakadiriwa kuongezeka maradufu ifikapo mwisho wa mwaka. “Tumekuwa na mwezi mmoja pekee wa mvua fupi tangu kuanza kwa mwaka wa 2020,” alisema Kitsao Kaingu, kiongozi wa jamii katika kijiji cha Tsangalaweni huko Ganze.

Wakati changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa, watoto walio katika mazingira na makazi duni ndio wanaoatharika zaidi!

https://www.standardmedia.co.ke/national/article/2001429517/hunger-pushes-children-out-of-class-to-seek-food-in-bushes-and-marriages

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *