Uchambuzi wa Mfumo wa Haki za Watoto Nchini Tanzania

By Martha Chimilila

Tanzania kama zilivyo nchi zingine duniani, inaendeshwa kwa kufuata misingi ya sheria, sera na katiba. Kuna vyombo mbalimbali ambavyo husimamia katiba na sheria mfano mahakama au vyombo vingine vya ulinzi.

Katika kutekeleza mikataba mbalimbali inayoletwa na nchi wahisani, mifumo ya sheria za watoto ilipimwa ili kuona ni jinsi gani inaweza kutumika vyema. Ikabainika kuwa, Sheria za Tanzania hazitoi ufafanuzi yakinifu kuhusu umri wa mtu. Ukisoma vifungu vya sheria vifuatavyo, unaweza ona utofauti na kandamizi kwa usimamizi wa haki za watoto;

   “Sheria ya Watoto na Vijana, cap. 13 ya 1937 iliyofanyiwa Mabadiliko, 1964 inafafanua kuwa mtoto ni mtu yoyote aliye chini ya miaka 12”

Sheria ya Kupitisha Watoto, kichwa namba 335, ya 1995, inasema kuwa, mtoto ni mtu yoyote aliye chini ya miaka 21 ambaye hajaoa au kuolewa”

Sheria ya Ndoa 1971 inasema msichana wa miaka 15 anaweza kuolewa kwa idhini ya Mzazi, wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, kama ilivyorekebishwa mnamo 1985, inasema mtu chini ya miaka 18 hawezi kupiga kura au kupigiwa kura”

Sheria ya Ajira, cap 366, inasema mtoto ni mtu yoyote ambaye yupo chini ya miaka 15”

Tanzania yaonyesha kwamba mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, kitamaduni na kisiasa, ambayo yamesababisha kuanzishwa kwa soko huria. Mabadiliko haya yameleta ongezeko la wahamiaji kutoka vijijini kwenda kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma. Hali hii ilisababisha watoto kuanza kujitegemea bila uangalizi wa wazazi na kusababisha kupotoka kwa maadili, na migongano na vyombo vya sheria. Hali hii ilichangia ongezeko kubwa la watoto wahalifu katika jamii.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimebaini, ahadi ndogo za kisiasa juu ya hitaji la kulinda ustawi wa haki na maslahi ya watoto nchini Tanzania. Serikali ya Tanzania imeshindwa kutekeleza kikamilifu majukumu ya usimamizi mzuri wa mifumo ya haki za watoto. Hii imejionesha katika Sheria ya Watoto na Vijana, sura ya 13, ambayo hairidhishiKwa kushindwa kuongeza au kuboresha, vifungu vya sheria za kulinda watoto wahalifu nchini Tanzania.

Mifumo ya haki za Watoto na Vijana Tanzania;

Vipengele vya mifumo ya haki za watoto na vijana nchini Tanzania, viko chini ya Mamlaka tofauti za mawaziri. Ustawi wa watoto na ulinzi kwa ujumla hushughulikiwa na Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Mfumo wa sheria upo chini ya Wizara ya sheria na katiba. Mahakama na Ofisi ya Jaji Mkuu zina uwezo wa kudhibiti uteuzi wa maafisa wa mahakama katika korti ya watoto.

Sheria ya watoto na Vijana ya mwaka 1973, sura ya 13, inasimamia matibabu ya watoto wanaokinzana na sheria” kwani ni sheria ya msingi kwa haki za watoto nchini Tanzania. Sura hii ya 13 inatumika kwa mtoto yoyote aliye chini ya miaka 16.

Mfumo wa Mahakama ya Vijana na watoto nchini Tanzania;

Mfumo wa mahakama nchini Tanzania una pande tatu ambazo ni;

  1. Mahakama ya rufaa
  2. Mahakama kuu
  3. Mahakama ndogo (zinajulikana kama mahakama za mahakimu 19 na mahakama za wadi 20)

Hukumu za Watoto na Vijana huanzia mahakama za watoto katika ngazi ya mahakama za wilaya na za mwanzo. Madhumuni ni kusikiliza na kuendesha mashtaka dhidi ya watu walio chini ya miaka 12, isipokuwa katika kesi ambazo watoto wanashtakiwa pamoja na watu wazima. Sheria nchini Tanzania inasema kwamba mahakama za watoto lazima ziketi jengo tofauti au kwa siku tofauti au nyakati tofauti kutokana na mahakama za Kawaida za watu wazima.

Mamlaka ya Mahakama za Watoto;

Mamlaka ya korti ya watoto ni pana na inatoa hukumu kwa kosa lolote isipokuwa mauaji au makosa ya jinai. Mamlaka ya korti za watoto inaendesha kesi zisizo za jinai, za watoto chini ya umri wa miaka 16 ambao wanahitaji ulinzi au nidhamu. Mnamo 1Julai 1998, umri wa uwajibikaji kwa makosa ya jinai nchini Tanzania ulibadilika kutoka miaka 7 hadi kufika 10. Hii ilitokana na hoja kua mtoto wa miaka kumi ana uwezo wa kutofautisha kati ya mema na mabaya.

Kwa sasa uwajibikaji wa jinai unaanzia miaka 10 hadi 12 ambapo unaenda sambamba na vifungu vingine vya sheria, ambavyo vinatambua watoto chini ya miaka 15, hawana uwezo wa kufanya maamuzi ya kupima athari na uzito wa jambo.

Nini kifanyike ili kuleta Usawa katika Mfumo wa Haki za Watoto

Kuboreshwa kwa sheria zitakazosimamia maswala ya haki za watoto. Sheria ambazo zitasimamia jinsi mtoto anapaswa kutibiwa katika jamii na vyombo vya kisheria. Nchi inapaswa Kutengeneza sheria za watoto ambazo zitaendana na Mikataba ya Haki za watoto na Mkataba wa Afrika.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *