Tumaini Njiani

By Martha Chimilila

Shule ya bweni ya wasichana pekee nchini Afghanistan, imesafirisha kundi kubwa la wanafunzi na wafanyakazi wake kwenda nchini Rwanda. Hatua hii, imechukuliwa siku chache baada ya kikundi cha Taliban kuiondoa serikali iliyokuwa madarakani nchini Afghanistan, kikundi hiki kinapinga wasichana na wanawake kupata elimu. 

Bi. Shabana Basij-Rasikh, Muanzilishi wa shule ya Uongozi Afghanistan (SOLA), ni Taasisi binafsi. Alifanya mahojiano na shirika la habari la CNN siku ya jumanne na kusema yafuatayo; 

“Wiki iliyopita tulisafirisha wanafunzi takribani 250 kutoka Kabul” 

“Watu wengi wako njiani kwenda nchini Rwanda kwa kutumia ndege za Shirika la Qatar. Lengo ni kuanza muhula mpya nje ya nchi kwa wanafunzi wetu” 

Makazi haya sio ya kudumu, hali ikitengemaa tunatarajia kurudi nyumbani. Ila kwa sasa ninaomba msaada kwa ajili ya jamii yangu”  

Bi Shabana alieleza, “Ilinibidi nichome moto rekodi zote za wanafunzi. Nilifanya hivyo nia sio kuzifuta bali ni kuwalinda wao na familia zao” 

Nilikuwa na miaka sita wakati Taliban waliingia madarakani. Niliogopa kwenda shule, sikutaka kuuawa na Talibani.Lakini wazazi walinisihi na kuniandikisha katika madarasa ya mtandaoni ili niweze kuendelea na elimu yangu.” 

“Baba yangu alinihimiza kwenda shule, kwa kuniambia unaweza poteza kila kitu katika maisha yako. Pesa inaweza kuibiwa, lakini jambo moja tu ambalo litabaki siku zote ni elimu. Elimu ni uwekezaji mkubwa sana katika maisha yako” 

“Hii ilinichochea kuanzisha SOLA (amani katika Lugha ya Kipashto), ili kuweza kuwasaidia watoto wa kike wa Afghanistani ambao hawana njia ya kupata elimu” 

Wizara ya Elimu nchini Rwanda imekubali kuikaribisha jamii ya SOLA katika mpango wao wa masomo. 

Source: https://edition.cnn.com/2021/08/25/africa/afghan-schoolgirls-semester-rwanda-intl/index.html 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *