Tuhuma za Mapenzi Baina ya Walimu na Wanafunzi

By Martha Chimilila

Katika kipindi cha miaka ya karibuni Tanzania imeona ongezeko kubwa la wanafunzi wa kike kuacha shule, tatizo kubwa ni kupata ujauzito. Mimba za utotoni katika miji mikubwa zimeongezeka kutoka watoto 3 kati ya 10 hadi watoto 7 kati ya 10. Tarehe 7 September 2021, Mkoani Dodoma Serikali ya Tanzania kupitia, Bi Ummy Mwalimu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imetangaza kuwafikisha walimu 285 kati ya 10,115 katika Tume ya Utumishi wa Ualimu kwa tuhuma za kujihusisha kimapenzi na wanafunzi katika kipindi cha miaka minne. 

“Makosa haya ni sawa na asilimia 2 ya makosa yote yaliyofika katika Tume ya Utumishi wa Ualimu. Tume hampaswi kumuonea mtu aibu endapo amevunja sheria” 

“Mwalimu yoyote atakayethibitika kuwa anajihusisha kimapenzi na mwanafunzi, kama serikali hatuta mvumilia na atachukuliwa hatua maana ni kinyume na sheria ya nchi na maadili ya kazi” 

“Viongozi wa Tume ya Ualimu, malalamiko ya walimu ni mengi sana, ni vyema kuyashughulikia kwa ufanisi na haraka” 

Waziri Ummy amesema alisema malalamiko mengi yalikuwa ni juu ya upandaji wa madaraja ambapo asilimia 96 wamepanda madaraja katika kipindi cha miaka mitano. Bi Ummy ameiagiza tume kuwa: 

Marufuku kubadilisha walimu tuliowapangia katika Halmashauri za nje ya miji bila kupeleka walimu wengine mbadala,” 

Source: https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/walimu-285-watuhumiwa-kujihusisha-kimapenzi-na-wanafunzi–3541706 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *