Kumekuwa na Tishio la Milipuko ya Magonjwa Hatari kutokana na kupungua kwa chanjo ya utotoni.
Kenya na mataifa mengine duniani yaliadhimisha Wiki ya Chanjo Duniani mnamo mwezi wa Aprili, Wiki ya mwisho.
Hata hivyo, kilicho wazi ni kwamba sekta ya afya lazima izingatie upya juhudi zake katika kampeni za chanjo ili kuwalinda watoto kutokana na hatari inayoongezeka ya kuambukizwa magonjwa ya zamani.
Tishio la kuibuka tena kwa magonjwa hatari ya utotoni kama vile nimonia, surua, kuhara, kifaduro, kifua kikuu, homa ya uti wa mgongo na polio imekuwa kweli katika miaka miwili iliyopita ya Covid-19, kwani mifumo ya afya ya ulimwengu imeelekeza umakini wao wote katika kupambana na virusi kwa gharama ya chanjo nyingine muhimu.
Kama matokeo ya janga hili, mifumo ya huduma ya afya ilielemewa na kukosa vifaa vya kutosha, na kampeni za chanjo hazikuwafikia watu waliozihitaji. Sambamba na hilo, mafuriko ya taarifa potofu yameondoa imani ya umma katika chanjo.
Kulingana na WHO, kiwango cha chanjo duniani kilipungua kutoka asilimia 86 mwaka 2019 hadi asilimia 83 mwaka 2020, huku takriban watoto milioni 23 walio chini ya mwaka mmoja wakikosa chanjo zao za kimsingi, hii ni idadi kubwa zaidi tangu mwaka wa 2009.
Kufikia mwaka wa 2020, idadi ya watoto ambao hawajachanjwa iliongezeka kwa milioni 3.4.
Ni mawasilisho 19 pekee ya chanjo yaliyoripotiwa mwaka wa 2020, ambayo ni chini ya nusu ya jumla ya miongo miwili iliyopita.
Aidha, wasichana milioni 1.6 zaidi hawakuwa na kinga kamili dhidi ya virusi vya papillomavirus ya binadamu (HPV) mwaka wa 2020 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Mnamo mwaka Jana, Wizara ya Afya ilionya kwamba, nchi iko katika hatari ya kuzuka kwa surua kutokana na kupungua kwa chanjo ya watoto,huku ikitaja milipuko katika maeneo ya Mandera, Wajir, Garissa, Pokot Magharibi na Tana River, hizi zikiwemo miongoni mwa kaunti zingine.
Wakati huo huo, wizara ya Afya ilisema kwamba, ni mtoto mmoja tu kati ya kila watoto watano anayepewa chanjo ya surua na rubela.
Pia kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watoto ambao hawajachanjwa, huku mrundikano wa watoto walio katika mazingira magumu ikifika zaidi ya milioni 2.1, huku janga la corona likizidi kuchochea madhara haya.
kulingana na WHO chanjo hulinda watoto na watu wazima dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika, pia huzuia magonjwa yanayodhoofisha, yanayolemaza na yanayoua.
Hii ikiunganishwa na afua zingine za kiafya kama vile uongezaji wa vitamini A ili kuongeza kinga ya watoto, dawa ya minyoo, ufuatiliaji wa ukuaji, na usambazaji wa vyandarua vilivyotiwa dawa ili kuzuia malaria, chanjo inakuwa na nguvu kubwa katika maisha ya mtoto.
Ni lazima tuboreshe elimu na mawasiliano kuhusu manufaa ya chanjo kwa walengwa. Kuna haja ya kuwahakikishia akina mama, kwa mfano, kwamba hospitali na zahanati bado ziko salama kutembelea na hazitawaweka kwenye hatari za kuambukizwa Covid-19.
WHO
Kampeni hizi zinaweza kufanywa kwa ushirikiano na viongozi wa jamii, mashirika ya serikali na yasiyo ya kiserikali, taasisi za kidini na redio za jamii.
Mwandishi-Khadija Mbesa