Wazazi

Nafasi za Kupendeza kwa Watoto, Rwanda

By Martha Chimilila Mfumo wa haki za watoto ni kitecho cha wazazi, jamii, serikali na wadau wanaosimamia na kulinda maswala ya watoto kama haki ya kupata elimu bora, lishe yenye tija na afya njema. Kuna mikataba mbalimbali duniani ambayo ilisainiwa kati ya nchi na Mashirika ya Kutetea na Kulinda haki za watoto duniani. Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda RIB imefungua nyumba maalum ambayo itatumika kusaidia watoto wawe na faraja, endapo watakuwa katika vyombo vya sheria kwa makosa mbalimbali. Watoto ambao wanawasiliana na mahakama ni wale ambao wanatuhuma za kuvunja sheria, waathirika na vitendo vya kuvunjwa kwa haki za watoto na mashahidi wa kesi mbalimbali. Ofisi ya Upelelezi nchini Rwanda wakishirikiana na UNICEF, siku ya jumatano september 15,2021, walizindua chumba rasmi kilichopewa jina la “Nafasi Rafiki kwa Watoto”, Chumba hicho kiko katika kituo cha Upelelezi Kicukiro katika wilaya

Nafasi za Kupendeza kwa Watoto, Rwanda Read More »

Wazazi katika Hatari ya Kukamatwa kwa kukosa Kusajili Watoto Kidato cha Kwanza

By Khadija Mbesa “Wazazi ambao hawataweza kuwasajili watoto wao kidato cha kwanza katika mkoa wa Pwani, wako katika hatari ya kukusanywa na serikali” alisema Mkuu wa mkoa wa Pwani bwana John Elungata(RC) Akizungumza katika kaunti ndogo ya Kinango ya Kwale, Elungata alisema kwamba, serikali haitasita kamwe, katika msukumo wake wa kufanikisha mabadiliko ya asilimia 100

Wazazi katika Hatari ya Kukamatwa kwa kukosa Kusajili Watoto Kidato cha Kwanza Read More »

Yatima katika Jamii

By Martha Chimilila Yatima ni mtoto aliyepoteza Mzazi mmoja ama wazazi wote, inaweza ikawa kwa ugonjwa au kitu kingine chochote. Tafiti zaonesha kuwa, zaidi ya watoto million 153 ni Yatima kwa kupoteza Mzazi mmoja, na takribani millioni 17.8 wamepoteza wazazi wote wawili. Visababishi vya mtengano kati ya watoto, wazazi na vituo vya kutoa misaada ni

Yatima katika Jamii Read More »