Sauti ya Jamii
By Martha Chimilila Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara nchini Tanzania, ni moja ya mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike. Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, alifanya ziara na kutembelea kituo cha Nyumba Salama cha Masanga kinachoendesha miradi ya kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Tarime. Dk. Gwajima alizungumza na waandishi wa magazeti mbalimbali ikiwemo gazeti la dijiti la Habari Leo, aliwaonya wananchi juu ya visingizio vya kuendeleza vitendo vya Unyanyasaji wa Kijinsia na uminywaji wa Haki ya kupata elimu kwa watoto wa kike. Dk. Gwajima alisema: “Jamii inapaswa kushiriki kikamilifu katika kufatilia matatizo yanayowasumbua wana jamii na iwapo watashindwa kufanya hivyo, basi watakuwa wanahusika kwa namna moja au nyingine katika kufanya vitendo hivyo” “Katika baadhi ya maeneo nchini, watoto wanafanyiwa vitendo vya kikatili na kukoseshwa haki ya kupata elimu, watumishi wa umma wanapaswa kuingilia kati swala hili ila wapo kimya. Baadhi ya watendaji […]