Elimu ni Chachu ya Maendeleo

By Martha Chimilila Mkoa wa Dar es Salaam, nchini Tanzania kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wa shule za msingi wanaorudia madarasa, katika shule za Serikali na zisizo za Kiserikali. Tafiti zinaonyesha kuwa idadi ya wanafunzi wanaorudia madarasa imeongezeka mara mbili zaidi katika kipindi cha miaka mitatu.  Ripoti iliyoandaliwa na Taasisi ya Elimu ya Msingi (Best) 2020, ilisomwa na Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ilionyesha ongezeko la wanafunzi wanaorudia madarasa katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2020.  Wadau wa Elimu walisema kuwa, kitendo cha kurudia darasa ni moja ya sababu zinazochangia wanafunzi kuacha shule. Kijana Felix Bitambo ni mmoja wa mwanafunzi aliyeacha shule na kuanza kufanya shughuli ndogo ndogo. Hii ilitokea baada ya kurudia darasa katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.   Felix alipoulizwa kwa nini aliacha shule alikuwa na haya …

Elimu ni Chachu ya Maendeleo Read More »