Ngono

Samaki Mkunje Angali Mbichi

By Martha Chimilila Tafiti zinaonyesha ongezeko kubwa la vijana walio athirika na ugonjwa wa Ukimwi nchini Tanzania. Hii imesababishwa na vijana wengi wadogo wenye umri chini ya miaka 15 kujihusisha na ngono. Tafiti zilizotolewa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids) zinaonyesha kuwa kwa Mikoa ya Dodoma na Tabora, inaongoza kuwa na asilimia kubwa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 wanaojihusisha ngono.  Dk. Pendo Saro, Mratibu wa Program ya Ongea wa Tume (Tacaids) alifanya mazungumzo siku ya jumamosi tarehe 11 September na waandishi wa habari, wakati wa Uzinduzi wa Program ya Ongea inayolenga kutoa elimu kwa vijana kuhusu Maambukizi ya Ukimwi na jinsi za kujikinga itakayokuwa inarushwa kupitia vipindi vya radio. Dk Penda alisema kuwa;  “Tafiti zinaonyesha kuwa vijana kati ya umri wa miaka 10 hadi 19 nchini Tanzania ni zaidi ya million 12. Asilimia 14 ni vijana wa kiume na asilimia 9 ni wa kike, wanajihusisha na ngono kabla hawajafika umri wa miaka 15. Asilimia 21.6 ya vijana walibainika kutokuwa na elimu yoyote kuhusu afya ya uzazi na Ukimwi. Hizi taarifa zimetolewa kwenye tafiti zilizofanywa nchini kuhusu masuala ya afya ya uzazi kati ya mwaka 2016/2017”  “Ijapokuwa tafiti zinaonyesha kuwa kadri vijana wanavyopatiwa elimu juu ya afya ya uzazi, idadi ya vijana wanaoshiriki ngono zembe katika umri mdogo inapungua ila kwa kasi ndogo sana”  “Kuna baadhi ya mikoa kama Dodoma (22%) na Tabora (20%) inaonyesha idadi kubwa ya vijana chini ya miaka 15, wakishiriki ngono zembe.”  Mhe. Ummy Ndeliananga, Naibu Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Ulemavu, alizindua program hii ya Ongea na kusema yafuatayo;  “Ni muhimu vijana kufatilia program mbalimbali na zenye maudhui ya afya za uzazi ili kuwasaidia katika kufanya maamuzi sahihi na kufikia ndoto zao. Tafiti mbalimbali zinaonyesha vijana wakipatiwa taarifa sahihi,elimu na huduma rafiki inawajengea uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha yao na kupunguza tabia hatarishi.”  Source: https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/watoto-mkoani-dodoma-tabora-waongoza-kuanza-ngono-chini-ya-miaka-15-3546850 

Kaa la Ukahaba Pwani

By Khadija Mbesa Ujana, Ngono na Utalii ni mambo ambayo yanaenda sambamba na yanapewa kipaumbele ndani ya roho ya Pwani Kenya. Mambo haya hayazingatii umri wala jinsia, watu wazima na hata Watoto wadogo wanaweza jipata ndani ya kisima hichi cha ukahaba. Mzazi kumfundisha mwanawe jinsi ya kujiuza na kupata fedha kupitia kufanya mapenzi na watalii …

Kaa la Ukahaba Pwani Read More »