Mtaji wa Maskini ni nguvu zake mwenyewe
By Martha Chimilila Vitendo vya imani potofu (ushirikina) ambavyo vinahusishwa na upatikanaji wa mali vimekuwa vikiongezeka katika baadhi ya maeneo ya vijiji nchini Tanzania. Katika Mji wa Mbulu, Mkoa wa Manyara, mtoto wa miaka 13 aliyefahamika kwa jina la Emmanuela Hhando aliuawa na baba yake mdogo anayejulikana kwa jina la Harold Hhando. Kitendo hiki kimetokea mara baada ya Bwana Harold kuoteshwa na mungu wake ya kuwa akila maini na viungo vya siri ya mtoto Emmanuela ataweza pata mazao mengi katika msimu huu wa kilimo. ACP Marrison Mwakyoma, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, aliongea na mwandishi wa gazeti la dijiti la Mwananchi kwa njia ya simu akisimulia: “Chanzo cha tukio hili ni imani za kishirikina, tumemuhoji Bwana Hhando ili kuweza kufahamu sababu za kufanya kitendo hiki cha kikatili, alisema kuwa aliambiwa na mungu […]
Mtaji wa Maskini ni nguvu zake mwenyewe Read More »