By Martha Chimilila Mfumo wa haki za watoto ni kitecho cha wazazi, jamii, serikali na wadau wanaosimamia na kulinda maswala ya watoto kama haki ya kupata elimu bora, lishe yenye tija na afya njema. Kuna mikataba mbalimbali duniani ambayo ilisainiwa kati ya nchi na Mashirika ya Kutetea na Kulinda haki za watoto duniani. Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda RIB imefungua nyumba maalum ambayo itatumika kusaidia watoto wawe na faraja, endapo watakuwa katika vyombo vya sheria kwa makosa mbalimbali. Watoto ambao wanawasiliana na mahakama ni wale ambao wanatuhuma za kuvunja sheria, waathirika na vitendo vya kuvunjwa kwa haki za watoto na mashahidi wa kesi mbalimbali. Ofisi ya Upelelezi nchini Rwanda wakishirikiana na UNICEF, siku ya jumatano september 15,2021, walizindua chumba rasmi kilichopewa jina la “Nafasi Rafiki kwa Watoto”, Chumba hicho kiko katika kituo cha Upelelezi Kicukiro katika wilaya