Siku ya Wanawake Duniani 2021

By Khadija Mbesah

#SelectToChallenge ni mandhari ya Siku ya Wanawake Duniani 2021. Hivi ndivyo unapaswa kujua. Mabadiliko yanatokana na changamoto – na ndio waandaaji wa ujumbe wa Siku ya Wanawake Duniani 2021 wanatarajia kupiga tarumbeta hivi leo. “Ulimwengu ulio na changamoto ni ulimwengu wa tahadhari,” tovuti ya Siku ya Wanawake Duniani inasema.

Wanawake wamekuwa mstari wa mbele kwa kuchangia katika uboreshaji wa teknolojia na hata katika mambo mengine mengi. Licha ya Imani potofu ya madai ya udhalili wa wanawake kwa wanaume, mada hiyo imeibuka kutokuwa na maana yeyote, kwani kila kukicha wanawake wanaoneka ni wenye nguvu na msimamo katika kuboresha na kujenga jamii.

Siku ya leo tunawasherehekea wanawake ambao wamepigana katika ulimwengu huu wa wanaume na kufanikiwa kuibuka kuwa washindi, na kuonyesha kuwa mada ya wanawake ni wanyonge na wadhaifu ni bali tu hadithi za kale na zisizo na ukweli wowote.

Leo ni siku ya kuwasherehekea wazazi wetu wa kike, dada zetu na wanawake wote wanaopigana kila siku ili kuweza kuwapa mwangaza Watoto wao katika Maisha ya baadaye, wanawake wote walioweza kutoka katika ndoa za unyanyasaji na madhalilisho.

wanawake ni washindi ndani ya nyumba zao, katika jamii na hata ulimwengu mzima. hongera kwa kuwa mwanamke na kuweza kupata nafasi mbele ya jamii ya leo.

 Wewe kama mwanamke, una uhodari, una ushujaa, uzuri na wewe ni baraka ndani ya hii dunia isiyokuwa na huruma. Leo tunakusherehekea.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *