By: Khadija Mbesah
I Am and I Will yaani “ninafanya na nitafanya” hii ni mandhari ya siku ya saratani duniani mwaka 2021, tunachukua fursa hii siku ya leo kuwapatia heko na kuwashangilia mashujaa ambao wamewashika mkono na kuwasaidia watu wote walioathirika na saratani wakati huu wa janga la COVID 19.
Janga la COVID-19 limeathiri vikundi vyote vya umri na kuna tofauti kwa watoto kutoka kwa watu wazima. Watoto wanaopata virusi wakati wanaugua saratani wanaweza kukabiliwa na changamoto za kipekee za kiafya kuliko wenzao. Utafiti huu ulilenga kuchunguza mitazamo ya watoto walio na saratani na familia zao katika enzi hii ya janga la COVID-19.
Mada kuu tatu zilitambuliwa kupitia uchambuzi wa mada.
1) kuzoea hofu na uoga hadi utakapozoea
2) kuachwa na upweke kwa sababu ya sheria ya kutotangamana na watu.
3) Kuchanganyikiwa kwa mfumo wa utunzaji, na kupungua kwa ubora wa huduma.
Janga la COVID-19 limelemea watoto wanaoishi na saratani na familia zao kwa njia tofauti. Uzoefu wao unaonyesha ufahamu mpya juu ya jinsi ya kuboresha maisha yao wakati huu mgumu.
Katika wakati huu mgumu Watoto wenye saratani wamekumbwa na majanga makubwa sana yakiwemo kutengwa, uoga na upekwe. Ila watu wengi wamewapa matumaini kupitia mitandao.
Huu mwaka tunatumai na tunaomba janga la COVID lipite, kwani nguvu na stamina ya kupiga vita pande mbili. Tuwapatie moyo na tuwe karibu na Watoto pia watu wakubwa walioathirika na saratani wakati huu wa janga la corona.
Je wewe umesaidia vipi Watoto walio na saratani katika kuwapa moyo na kuwashikana mkono wakati huu wa janga la COVID 19?
follow us on
Twitter:https://twitter.com/mtotonews
subscribe to our YouTube channel:https://YouTube.com/mtotonewstv
Mtoto News is a Digital Online platform of news, information and resources that aims at making significant changes in the lives of children by making them visible. Read mtotonews.com or follow us on Twitter and Facebook@mtotonewsblog
[url=http://slkjfdf.net/]Ipaepolu[/url] Iwtemiq qdp.bxhe.mtotonews.com.kmd.aw http://slkjfdf.net/