Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike

By Khadija Mbesa

Ufikiaji wa elimu, huduma za afya, vifaa vya kujifunzia vyenye ustadi, fursa sawa, kinga dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia na ubaguzi ni mada za kawaida ambazo hufanyiwa kazi mwaka baada ya mwaka. Kulingana na kaulimbiu ya mwaka huu, ni Kizazi cha digiti, kizazi chetu.

Lengo kuu ni kuziba mgawanyiko wa dijiti. Kulingana na Umoja wa Mataifa, hasa katika ulimwengu , baada ya COVID-19 ambao waliona biashara, elimu na hata sehemu za huduma za afya zikihamia mkondoni.Hii ikikadiria kwamba,” watu bilioni 2.2 walio chini ya umri wa miaka 25 bado hawana Intaneti nyumbani. ”

Ripoti hiyo pia ilibaini kwamba, wasichana wana uwezekano mkubwa wa kuachwa nyuma, hii ikionyesha mgawanyiko wa kijinsia ndani ya mgawanyiko wa dijiti. Pia ilisemekana kwamba, wasichana wana uwezekano mdogo kuliko wavulana wa”kutumia na kumiliki vifaa.” Hii, kwa upande wake, inaathiri idadi yao katika “ujuzi na kazi zinazohusiana na teknolojia”.

Mnamo 2021, Jukwaa la Usawa wa Kizazi lilizindua ahadi za miaka mitano kwa suluhisho kali za usawa wa kijinsia – kama vile ulimwengu uliingia mwaka wa pili wa janga la COVID-19. 

Mwaka huu, tunapigania fursa sawa katika jinsia zote, kwenye nafasi za kutumia digiti, na kuboresha uafikiaji wa teknolojia kwa kila mtoto.Advertisementsabout:blank

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *