Sauti ya Jamii

By Martha Chimilila

Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara nchini Tanzania, ni moja ya mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike. Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, alifanya ziara na kutembelea kituo cha Nyumba Salama cha Masanga kinachoendesha miradi ya kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Tarime. 

Dk. Gwajima alizungumza na waandishi wa magazeti mbalimbali ikiwemo gazeti la dijiti la Habari Leo, aliwaonya wananchi juu ya visingizio vya kuendeleza vitendo vya Unyanyasaji wa Kijinsia na uminywaji wa Haki ya kupata elimu kwa watoto wa kike. 

Dk. Gwajima alisema: “Jamii inapaswa kushiriki kikamilifu katika kufatilia matatizo yanayowasumbua wana jamii na iwapo watashindwa kufanya hivyo, basi watakuwa wanahusika kwa namna moja au nyingine katika kufanya vitendo hivyo” 

Katika baadhi ya maeneo nchini, watoto wanafanyiwa vitendo vya kikatili na kukoseshwa haki ya kupata elimu, watumishi wa umma wanapaswa kuingilia kati swala hili ila wapo kimya. Baadhi ya watendaji katika ngazi mbalimbali hawafanyi kazi wanayopaswa kufanya na tuna walipa mshahara wa bure” 

Watendaji wa Mtaa, Kata Mkoani Mwanza anapoishi mtoto aliyekoseshwa haki ya kwenda shule, mtoto mwenye umri wa miaka tisa. Watendaji mpo kimya mkisubiri ndugu zake wafike, nakuja kuzungumza nanyi” 

Dk. Gwajimaaliwahasa wananchi na kusema kuwa “Vitendo vya ukeketaji vitaweza kukomeshwa endapo wanaume watakaa chini na Kujadili hili tatizo. wasiishie Kujadili tu ila wapaze sauti za kukataa vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike” 

Bwana Valerian Mgani, Meneja Mradi wa Kupinga Unyanyasaji wa Jinsiaakiwa anasomataarifa ya kituo hicho alisema kuwa,“Kituo cha Nyumba Salama ya Masanga kilianzishwa mwaka 2006 na kupata usajili 2015 ikiwa na lengo la kuwasaidia watoto waliopata tatizo la Ukatili wa Kijinsia ikiwemo ukeketaji. Kwa sasa kituo kinatoa huduma kwa watoto 34, ambapo wakiume ni mmoja” 

‘Katika kituo chetu tunakabiliwa na changamoto ya bweni, chombo cha usafiri na watoto wa kike kukatishwa masomo sababu ya ukeketaji na mimba za utotoni’ 

Source: https://www.habarileo.co.tz/habari/2021-08-18611d25e512093.aspx 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *