Onyo kwa Wazazi Wanaowanyima Watoto Haki ya Kupata Elimu

By Khadija Mbesa

Viongozi kutoka Ashabito, Mandera Kaskazini wamewaonya wazazi na walezi dhidi ya kuwanyima watoto wao haki ya kupata elimu wakisema kuwa siku zao zimehesabiwa.

Akiongea katika hafla huko Ashabito, mkuu wa eneo la Morothile Abiy Jillo alisema elimu ni ufunguo wa maisha yenye mafanikio na kusisitiza kwamba jamii isiyo na elimu ni sawa na jamii isiyo na mbele wala mwisho.

“Serikali imetoa elimu ya bure katika shule yetu ya msingi, kwa hivyo hakuna mtu aliye na kisingizio cha kutochukua watoto wao ili waweze kupata elimu ya msingi,” alisema Jillo.

Chifu Jillo, alishutumu usajili mdogo wa msingi katika eneo hilo, akionya wazazi ambao wanapuuza majukumu yao ya uzazi kuwa, watakabiliwa na ghadhabu kamili ya sheria. Alionya wazazi na walezi kwamba, iwapo yeyote anayehusika katika ndoa za mapema pia atakabiliwa na sheria.

Aliwataka wazazi kuwapeleka watoto walemavu shuleni kwani ulemavu sio kutokuwa na uwezo.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Morothile Osman Mohammed aliwaambia wazazi kwamba watoto wanahitaji elimu ya msingi ili kuweza kuelewa na kueneza dini ya kiislamu kwa wengine.

“Tusizingatie elimu ya madrasa tu, watoto wetu wana haki ya kupata elimu ya msingi na lazima tuhakikishe wanapata,” alisema Osman.

Sharmake Gulie MCA pia alisisitiza kuwa, watoto wote, bila kujali jinsia na kabila lazima wapewe elimu.

Aliiomba serikali ichukue hatua dhidi ya wazazi na walezi ambao hawapeleki watoto wao shule.

Asilimia nzuri ya wazazi huko Mandera wanapendelea watoto wao kuwa na elimu ya Madrasa (Thugsi) kuliko elimu ya msingi ya Kenya.

https://www.kenyanews.go.ke/parents-warned-against-denying-children-right-to-education/

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *