By Khadija Mbesa
Wakati nchi zililazimishwa kufungwa ili kuzuia kuenea kwa SARS-CoV-2, shule zilifungwa na wakati wa skrini ya watoto uliongezeka. Pamoja na madarasa yanayofundishwa mkondoni, na amri za kutotoka nje zilizoanzishwa katika nchi zingine, watoto walikuwa wakitumia muda zaidi na zaidi ndani ya nyumba.
Hili lilisababisha wao kutumia wakati wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii, Utafiti wa zaidi ya watoto 6,000 wenye umri wa miaka 10-18 kutoka Juni hadi Agosti mwaka jana uligundua kuwa karibu 50% ya watoto walipata angalau aina moja ya uonevu wa kimtandao katika maisha yao, kulingana na ripoti ya https://ec.europa.eu/jrc/en/publication/how-children-10-18-experienced-online-risks-during-covid-19-lockdown-spring-2020
Uonevu wa mitandao ni ngumu sana kuepukwa, kwani imejawa na maono ya watu ambao wako nyuma ya kibodi na kazi yao ni kutupa maneno yasiyo na msingi na ya maonevu na matusi na unyanyasaji.
Utafiti wa Afrika Kusini uliochapishwa katika Jarida la Kimataifa la Uhalifu na Sosholojia, https://www.lifescienceglobal.com/pms/index.php/ijcs/article/view/7165
uligundua kuwa kuongezeka kwa matumizi ya mitandao ya kijamii wakati wa kufungiwa kumesababisha watoto wengi na vijana kuwa wahanga wa unyanyasaji wa mtandao, pamoja na maoni ya kijinsia kwenye picha za wanawake wachanga, watu wakitukanana, na video za watoto wa shule wanapigana. Utafiti huo ulionyesha matumizi ya akaunti bandia kuwanyanyasa wengine.
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeelezea uonevu kama shida kubwa ya afya ya umma. Inaweza kusababisha unyogovu, wasiwasi na wakati mwingine kujiua. Inaweza pia kusababisha utumiaji mbaya wa dawa za kulevya, kujitoa kijamii, kukosa kwenda shule au kuacha masomo, na inaweza kuwa na athari baadaye maishani.
Je, wewe kama mtumizi wa mitandao, utasaidia vipi katika kupunguza athari za uonevu na unyanyasaji wa Watoto katika mitandao ya kijamii? Tafakari.