Nafasi za Kupendeza kwa Watoto, Rwanda

By Martha Chimilila

Mfumo wa haki za watoto ni kitecho cha wazazi, jamii, serikali na wadau wanaosimamia na kulinda maswala ya watoto kama haki ya kupata elimu bora, lishe yenye tija na afya njema.

Kuna mikataba mbalimbali duniani ambayo ilisainiwa kati ya nchi na Mashirika ya Kutetea na Kulinda haki za watoto duniani. Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda RIB imefungua nyumba maalum ambayo itatumika kusaidia watoto wawe na faraja, endapo watakuwa katika vyombo vya sheria kwa makosa mbalimbali.

Watoto ambao wanawasiliana na mahakama ni wale ambao wanatuhuma za kuvunja sheria, waathirika na vitendo vya kuvunjwa kwa haki za watoto na mashahidi wa kesi mbalimbali. Ofisi ya Upelelezi nchini Rwanda wakishirikiana na UNICEF, siku ya jumatano september 15,2021, walizindua chumba rasmi kilichopewa jina la “Nafasi Rafiki kwa Watoto”, Chumba hicho kiko katika kituo cha Upelelezi Kicukiro katika wilaya ya Kicukiro. 

Isabelle Kalihangabo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Upelelezi Rwanda, aliwaambia waandishi wa habari kuwa: 

“Zaidi ya watoto 2000 kila mwaka wanaripotiwa kuwa na migogoro na sheria. Lakini hakukuwa na vyumba rafiki kwa watoto kucheza katika kipindi wanachosubiria tamko kutoka mahakamani. Nafasi hizi zitasaidia watoto wanaokuja kwetu kwa makosa tofauti na vitasaidia katika kubadilishana uzoefu na ushuhuda wakati wa uchunguzi,”  

“Hii nafasi ya watoto pia itatusaidia katika usimamizi mzuri wa kesi za watoto wanaokinzana na sheria” 

“Kuna nafasi nyingine zinatarajiwa kukamilika maeneo ya Kaskazini mwa nchi,lakini nafasi hizi zinapaswa kuanzishwa nchi nzima. Hatua hii inaambatana na ulinzi wa watoto kwa kutumia mtaalamu na uchunguzi yakinifu wa makosa ya kihalifu kwa watoto na kutengeneza mazingira rafiki.” 

Bi.Julianna Lindsey, Mwakilishi wa UNICEF nchini Rwanda, alisema kuwa; 

“Nafasi hizi zinahitaji maboresho ya miundombinu na vifaa rafiki ambavyo vitasaidia wakati wa kufanya mahojiano. Inapaswa kuwa na wachunguzi waliopata mafunzo ya kuchukua video, wakati mahojiano yakiendelea ambayo yatatumika mahamakani. Nafasi hizi zitapunguza majeraha ya hisia kwa watoto ambayo yanasababishwa na hali ya kurudia video katika kipindi cha kutoa ushahidi mahakamani.Hii itahakikisha kufanikiwa kwa mashtaka ya kesi zinazohusu watoto kwa sababu ushahidi uliorekodiwa unaweza kutumika katika chumba cha korti kwa njia bora” 

Source: https://www.newtimes.co.rw/news/rib-introduces-child-friendly-spaces 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *