Mtaji wa Maskini ni nguvu zake mwenyewe

By Martha Chimilila

Vitendo vya imani potofu (ushirikina) ambavyo vinahusishwa na upatikanaji wa mali vimekuwa vikiongezeka katika baadhi ya maeneo ya vijiji nchini Tanzania. Katika Mji wa Mbulu, Mkoa wa Manyara, mtoto wa miaka 13 aliyefahamika kwa jina la Emmanuela Hhando aliuawa na baba yake mdogo anayejulikana kwa jina la Harold Hhando. Kitendo hiki kimetokea mara baada ya Bwana Harold kuoteshwa na mungu wake ya kuwa akila maini na viungo vya siri ya mtoto Emmanuela ataweza pata mazao mengi katika msimu huu wa kilimo. 

ACP Marrison Mwakyoma, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, aliongea na mwandishi wa gazeti la dijiti la Mwananchi kwa njia ya simu akisimulia: 

“Chanzo cha tukio hili ni imani za kishirikina, tumemuhoji Bwana Hhando ili kuweza kufahamu sababu za kufanya kitendo hiki cha kikatili, alisema kuwa aliambiwa na mungu wake katika ndoto kuwa amuue mtoto wa kaka yake na kula maini ili avune mazao mengi. Hhando alikuwa ni mkulima katika eneo la Silaloda, ila imani za kishirikina zimesababisha kumuua mtoto wa kaka yake kwa kumpasua na kuchukua viungo vya siri na maini. Kwa sasa Bwana Hhando yupo chini ya ulinzi wa polisi huku Taratibu nyingine za kisheria zikiendelea.” 

“Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Manyara, naomba tuepuke imani za kishirikina zinazosababisha mauaji ya kikatili na kufanya kazi kwa bidi ili tuweze kupata faida tunayotarajia” 

Mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Silaloda, aliyetambulika kwa majina ya Johna Baynetalisema kuwa; “Sisi wananchi wa eneo hilo tumesikitishwa na kitendo cha kikatili alichokifanya Bwana Hhando kwa kumuua binti mdogo kwa tamaa zake za mali. Bwana Hhando hakuwa na rekodi yoyote ya matukio ya kihalifu katika mtaa wetu” 

Source: https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/mbaroni-kwa-tuhuma-za-kumuua-mtoto-wa-kaka-yake-3521090 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *