By Khadija Mbesa
Hebu tuseme kwa mfano, wewe kama mzazi uko katika mitandao ya kijamii kama vile Instagram na Twitter, alafu pia mwanao ako katika mitandao hiyo hiyo ya kijamii na anaweza kuona chochote unachochapisha ndani ya mitandao. je? mtoto wako atachukulia vipi mwonekano wako kwake atakapoona picha au ambazo unachapisha kwa ukurasa wako hazina heshima wala adabu hata kidogo? Tujadili.
Watoto wengi hukosa kuwapa heshima wazazi wao kwa sababu ya jinsi wazazi hao wanajibeba na kujieka kwenye jamii. Unaweza pata mzazi wa kike ambae hana bwana lakini ana Watoto, wacha tuseme ni single parent, anachapisha picha zisizokuwa na heshima na mpenzi wake kwenye mitandao, haswa huu wakati wa siku ya wapendanao. Basi mtoto anaweza ona picha hizo na yeye akadhani ni jambo la kawaida kabisa.
Katika maandishi yangu ya zamani nakumbuka nikieleza ya kwamba mitandao ya kijamii inaweza kuwa na manufaa na pia inaweza kuwa na balaa. Ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya mitandao, Nyumba zimekuwa moto kwa matoelewano na chazo ni mitandao.
Juzi tu nimeona mama mzima akisema ya kwamba mtoto wake wa miaka 19 ameleweshwa na kuchukuliwa picha chafu na zikawekwa mitandaoni. Lakini ukiangalia kwa undani unapata mtoto huyo amelelewa ndani ya mitandao, yani amewekwa wazi mbele ya mitandao na mzazi wake. Huyo mama mwenyewe ukiangalia ukurasa wake katika mitandao basi unaweza sikitika mno. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo jamani. Hebu tujaribu tujirekebisha sisi wenyewe kabla ya kulaumu mwengine kwa sababu ya makosa ya Watoto wetu ama visa vinavyowatokea Watoto wetu. Wewe kama mzaz utachapisha aje vitu visivyokuwa na heshima mitandaoni, huku ukienda kujinafasi na huyo mtoto wako wa kike nab ado unachapisha vitu hivyo mitandaoni? Mimi bado sijaweza kukubaliana na hili. Wewe kama mzazi wa kike unafaa kuwa na kipau mbele kwa kumlinda mtoto wako dhidi ya shida na michepuko ya mitandao, lakini kwa sababu ya pupa yako ya kupata umaarufu mitandaoni basi unaweka wazi mitandao mbele ya mwanao bila hata kumsimamia ili kuona ni nini hasa anafanya mitandaoni.
Hivi ni kwa nini mwanzo tunahimiza Watoto wakuwe na kurasa katika mitandao ya kijamii. Mwanzo siku hizi mitandao mingi ya kijamii imejaa picha chafu mno bila ya kutaka kujua kama kuna Watoto wenye umri mdogo sana. Na kama unahimiza sana mtoto wako akuwe mtandaoni basi hakikisha ukurasa wake unafwatiliwa na wewe kama mzazi.
Dunia imekuwa haina usalama mbele ya Watoto, tafadhali wewe kama mzazi jaribu kujitahidi kutokua chanzo cha kukosa heshima mbele ya mwanao na pia usiwe chazo cha kuwa muozo wa jamii mbele ya mtoto wako.
follow us on
Twitter:https://twitter.com/mtotonews
subscribe to our YouTube channel:https://YouTube.com/mtotonewstv
Mtoto News is a Digital Online platform of news, information and resources that aims at making significant changes in the lives of children by making them visible. Read mtotonews.com or follow us on Twitter and Facebook@mtotonewsblog