Migogoro ya Hali ya Hewa na Ustawi wa Watoto

By Martha Chimilila

Mabadiliko ya hali ya hewa yanaleta athari kubwa ulimwenguni, na kusababisha athari kwa kizazi cha sasa na baadae. Mabadiliko ya hali ya hewa yanahusishwa na tatizo la ukosefu wa usawa na uminywaji wa haki, watoto wengi katika nchi zinazoendelea na kaya maskini watapata athari kubwa kuliko wengine. Athari zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa watoto sio nadharia bali ni ukweli na zinahitaji Utatuzi wa haraka. 

Taasisi ya Save the Children ikishirikiana na timu ya Kimataifa inayoongoza tafiti duniani, walifanya tafiti juu ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa watoto. Taasisi ya Save the Children imechapisha ripoti iliyohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 12 hadi 17, ili kuweza kufahamu athari za mabadiliko ya hali ya hewa zinavyokiuka haki za watoto za kuishi, elimu na ulinzi. Tafiti hii ilisaidia kujua kwa kiwango gani watoto wanathirika na mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na; 

“Umuhimu wa Kupunguza uzalishaji wa kiwango cha joto hadi kufikia 1.5c katika viwango vya awali vya Viwanda. Kuweka maslahi ya watoto kama kipaumbele cha kwanza, itaweza kupunguza hatari kubwa ya migogoro ya hali ya hewa katika siku za mbeleni. Watoto wanathirika na matatizo ambayo hawajayatengeneza”  

“Mlango wa kufanya mabadiliko ya tabia ili kuweza kulinda maslahi ya watoto umeanza kujifunga taratibu. Hali ya kujitolea katika kuchukua hatua dhidi ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa na fedha bado hazina uwezo wa kutosha, kama viongozi wa ulimwengu wataongeza matamanio yao basi kizazi kijacho kitateseka zaidi” 

Nini kifanyike ili kuweza kupunguza tatizo:  

Serikali, wananchi na wanaharakati wa maswala ya watoto wana jukumu la kutengeneza sera za kupunguza kiwango cha joto duniani ikiwa pamoja na utumiaji wa mafuta ya asili. 

Ushiriki wa watoto katika kutoa hoja na maamuzi juu ya mabadiliko ya hali ya hewa. Watoto ni washikadau wa kwanza na muhimu katika kushughulikia tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa, na kuanzisha mifumo na majukwaa mbalimbali ya kujadili kuhusu tatizo hili. 

Kuongeza mifumo ya ulinzi wa jamii katika kusaidia familia na watoto, katika Kutatua tatizo la athari za mabadiliko ya hali ya hewa na Uboreshaji wa ustawi wa watoto. 

Source: https://resourcecentre.savethechildren.net/library/born-climate-crisis-why-we-must-act-now-secure-childrens-rights?_ga=2.92230682.1214076089.1632479803-2133679589.1567418591 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *