By Khadija Mbesa
Sheria ya kiislamu, sheria ya kimila, na sheria ya jinai ya kidunia inatumika nchini Somalia, ila hakukuwa na sheria madhubuti, inayofanya kazi ya kitaifa na hakuna marufuku wazi ya adhabu ya kifo, adhabu ya viboko au kifungo cha maisha kwa wakosaji watoto kote nchini.
Sheria ya Mpito ya Shirikisho (TFG) ni serikali inayotambuliwa kimataifa ya Somalia. Mnamo 2009, Bunge la Shirikisho la Mpito, lilipiga kura ili kutekeleza sharia kama sheria ya kitaifa. Kulingana na Rais aliyechaguliwa enzi hizo, hii itakuwa tafsiri ya wastani ya ‘Sharia’. Walakini, TFG inadhibiti sehemu kidogo ya mjii mkuu wa Mogadishu, Maeneo mengine kusini mwa Somalia yapo chini ya vikundi vya upinzani venye silaha, haswa Alshabab na Hizbul Islam, ambazo zinaweka tafsiri kali ya sheria ya kiislamu.
Kaskazini, mkoa unaojitawala wa Puntland na jamhuri ya kujitegemea ya Somaliland ina utulivu zaidi, na serikali zinazofanya kazi na mifumo ya sheria.
Hakuna umri wa chini kabisa, wa uwajibikaji wa jinai nchini Somalia. Kulingana na Kusini au Kati mwa somalia na Puntland, kanuni ya adhabu ya somalia 1962 inaweka umri wa chini wa uwajibikaji wa jinai, miaka 14 na inatoa adhabu iliyotengenezwa kwa watoto wenye umri wa miaka 14 hadi 17. Mahakama ya watoto na sheria ya marekebisho 1970, inafafanua mtoto kama chini ya miaka 14, na kijana kama 14-17. Mahakama hiyo yasema kwamba, korti ya watoto ina mamlaka ya kipekee, ya kusikiliza na kuamua kesi zinazohusiana na watoto pamoja na vijana kuhusu kosa lolote lile, isipokuwa mauaji.
Walakini, inawezekana kwamba, sheria hii haijawahi kutekelezwa na sheria mpya ya watoto inaripotiwa kutungwa huko Puntland. Sehemu ya Somaliland, sheria ya vijana 2007, inaweka umri wa uwajibikaji wa jinai kuwa miaka 15, na inalinganisha vifungu vya sheria ya kidunia, na sheria ya kitamaduni. Walakini, sheria haijatekelezwa kikamilifu na kazi nyingi za korti za chini, katika haki za jinai.
Mambo, haswa yanayohusu watoto, yametekelezwa hivi karibuni na kamati za usalama za mkoa. Wakati wa miaka ya 1980, hukumu zilizotolewa na kamati hizi, ni pamoja na kifungo cha maisha na adhabu ya kifo, japokuwa hivi karibuni, sheria hizo zinaonekana kuwa duni.
(Source 1 )
Hivi sasa, mfumo wa kisheria unaosimamia watoto wanaokinzana na sheria umepitwa na wakati, na hauambatani na mkataba wa haki za Mtoto na vyombo vyovyote vinavyotumika vya kimataifa.
Sheria ya vijana ya 1970 ndio kifungu maalum pekee ndani ya mfumo wa sheria ya Somalia, ambao unasimamia matibabu na usimamizi na kuwekwa kizuizini kwa watoto, ndani ya mfumo wa haki ya jinai.
Kama nilivyosema hapo awali, Somalia haikuwa chama cha Mkataba wa haki za Mtoto (CRC) au itifaki zake za hiari enzi hizo.
Chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya adhabu, watoto walio chini ya umri wa miaka 14 hawatakuwa na jukumu la jinai. Umri wa uwajibikaji kwa hivyo huanza baada ya miaka 14.
Hakuna vifungu maalum vinavyoongoza matibabu kwa watoto walioko gerezani, au tawala maalum kwa watoto walioko kizuizini. Walakini, kifungu cha 60 cha sheria hiyo hiyo kinasema kwamba, watoto walio na miaka 14 hadi 18, wanapelekwa gerezani ikiwa wamekamatwa au wamehukumiwa kosa kubwa, ila wakati wa tathmini, mamlaka ya Somalia haikutoa ufafanuzi wowote kuhusu ni kosa gani lililo kubwa.
Kwa hivyo, kuna pengo katika sheria inayotumika kuhusu umri ambao mtoto anaweza kupelekwa gerezani au kuwekwa kizuizini. Mwisho kabisa, watoto waliopatikana na hatia ya makosa madogo, wanaweza kuachwa kwa msamaha ikiwa dhamana itatolewa.
Ijapokuwa Somalia haikuwa mwanachama wa Mkataba wa Haki za Watoto, mnamo mwaka wa 2015 Somalia ilifanya historia kwa kutekeleza haki za watoto kwa kuwa nchi ya 196 katika kuridhia Mkataba wa Haki za Mtoto (CRC).