Mchezo wa Mtandaoni Utakaokuza Jukwaa la Usalama Kwa Watoto

Khadija Mbesa

Februari, 2022. Nairobi Kenya

Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CAK) imezindua rasmi mchezo wa mtandaoni unaoitwa  ‘Cyber ​​Soldjas’  kwa minajili ya kukuza jukwaa salama la mtandaoni kwa watoto.

Akizungumza katika hoteli moja, hapo jana jijini Nairobi, Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa CAK, Mercy Wanjau, alisema kwamba, mchezo huo wa mtandaoni unalenga watoto wenye umri wa kati ya miaka 4 hadi 14, akiongeza kuwa, watoto wa rika hili watapata uzoefu bora kupitia vitendo na kurudia.

“Mchezo huu unalenga kuwaongoza watoto kupitia msururu wa hatari zinazoweza kutokea mtandaoni, na pia kuwafundisha jinsi ya kulinda utambulisho wao, data ya kibinafsi, kutambua tovuti zilizo na maudhui hatari na hatimaye kubuni mbinu muhimu kuhusu taarifa zinazopatikana kwenye mtandao,” alisema Wanjau.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, mchezo huo una viwango vitano kulingana na udhaifu na hatari zilizopo kwenye mtandao, ikiwa ni pamoja na uhalifu wa mtandao, wizi wa vitambulisho, habari za uongo na uvuvi wa kamba.

Hata hivyo, alibainisha kwamba, kuongezeka kwa upatikanaji wa intaneti na teknolojia ya kidijitali pia kunaleta changamoto kubwa kwa watoto na vijana ikiwemo usalama wao.

“Athari huanza kutoka matishio, hadi ikafikia ulinzi wa data ya kibinafsi, uonevu mtandaoni, maudhui hatari ya mtandaoni, nia ya ngono na unyonyaji,” alisema Wanjau.

Mchezo wa mtandaoni utakamilisha mipango mingine ya awali kama vile Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni (COP) ili kuunda mtandao salama kwa watoto.

Mamlaka imepitisha mbinu ya washikadau mbalimbali, ili kuhakikisha kwamba, watoto na vizazi vijavyo wanalindwa na kuwezeshwa kustawi katika mazingira ya kidijitali.

Tunatoa programu za mafunzo ya ustadi wa kidijitali zinazojumuisha usalama mtandaoni kwa mfano, DigiTruck ambayo inalenga vijana wasio na huduma haswa kutoka jamii zilizo mashambani, inayofundisha usalama mtandaoni kila siku, pamoja na washirika wengine

MKURUGENZI WA WANAWAKE KATIKA TEKNOLOJIA SHIRIKA LA HUAWEI
– KENYA, MAUREEN MWANIKI

Uzinduzi huo unakuja wakati ulimwengu unaadhimisha, Siku ya Mtandao Salama, ambayo ilianza kama mpango wa Mradi wa Mipaka Salama wa Umoja wa Ulaya mnamo mwaka 2004.

Kenya News

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *