Maziwa ya Mama

By Martha Chimilila

Bi. Ruthi Mkopi, Afisa wa Utafiti, Mwandamizi Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, alizungumza na waandishi wa gazeti la Habari leo akisema “Asilimia 58 kati ya 100, ya watoto walio chini ya miezi sita ndiyo wanaonyonya Maziwa ya mama zao” Hii inaonyesha kuwa asilimia 42 ya watoto hawanyonyi Maziwa ya mama zao sababu ya Ugonjwa wa Uviko 19. 

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani hadi sasa hakuna Ushahidi wa Kiutafiti kuhusu uwepo wa maaambukizi ya virusi vya Uviko 19 kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kipindi cha mimba au kupitia Maziwa katika kipindi cha unyonyeshaji’ 

Pia Bi Ruthi alitoa ushauri na kusema” Napenda kuwasihi wanawake Wanaonyonyesha kuwa katika kipindi hiki cha mapambano zidi ya janga la Uviko 19, ni muhimu kuendelea kufata maelekezo yanayotolewa na Wataalamu wa afya ili kuweza kuwalinda watoto wanaonyonya” 

Ni vizuri kulinda afya za watoto walio chini ya miezi sita ili kuwalinda na magonjwa mbalimbali. Hii itawezekana kwa kuepuka kuwapa watoto Maziwa ya makopo yanayouzwa madukani” 

Source:  https://www.habarileo.co.tz/habari/2021-08-16611a5547045a5.aspx 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *