Mazingira ni Kesho ya Watoto Wetu

By Martha Chimilila

Hali ya Hewa ni wastani wa mabadiliko ya sehemu husika katika miaka mingi.  

Dunia kwa sasa iko katika kipindi cha Mabadiliko ya hali ya hewa ya haraka haswa kupanda kwa joto. Mabadiliko ya hali ya hewa imebadilisha utaratibu wa maisha na kusababisha ukame, kuongezeka kwa kina cha maji katika baadhi ya maeneo na upungufu wa chakula. Ulimwengu kwa sasa umepata joto kwa asilimia ya 1.2C tangu kuanza mapinduzi ya viwanda yalipoanza na joto litaendelea kuongezeka kama serikali hazitafanya jitihada za kupunguza tatizo hili. 

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imethibitisha ongezeko la mabadiliko ya hali hewa na kusababisha majanga katika karne ya 21. Baadhi ya maeneo yanaweza kuwa na joto hatari na maeneo mengine hayafai kwa makazi sababu ya ongezeko la viwango vya maji. Moja ya ripoti iliyotolewa na shirika la Save the Children nchini Burundi, ni kuongezeka kwa maji katika Ziwa Tanganyika na kusababisha takribani familia 100,000 kuhama makazi yao. Watu katika nchi masikini, ambazo zina uwezo mdogo wa kubadilika, wanateseka zaidi. 

Mtoto wa miaka 17 nchini Burundi aliongea na Shirika la Save the Children na kuelezea yaliyotokea: 

“Ilikuwa usiku sana, wote tukiwa tumelala na niliamka nikapata maji yamejaa ndani ya nyumba. Nyumba iliharibika muda mfupi baada ya kuiacha” 

Takribani 85% ya watu wanaoishi katika kambi nchini Burundi wamehama kutokana na majanga ya asili, yaliyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Watoto ndiyo waathirika wakubwa wa majanga hayo, watoto 7200 ni chini ya mwaka mmoja wanaishi katika kambi ambapo wanakosa huduma muhimu kama afya na malazi. Mmoja wa wafanyakazi wa shirika la Save the Children alisema kuwa: 

“Katika Kambi ya Gatumba kuna jumla ya wakazi 3,000 na asilimia 80 ya wakazi hao ni watoto. Wengi hawapati elimu na wanakula mlo mmoja tu kwa siku” 

Nini kifanyike kupunguza tatizo hilo: 

Kutengeneza vyanzo vya nishati mbadala kama kupunguza matumizi ya magari na kutumia usafiri wa baiskeli. 

Serikali zinashauriwa kutengeneza sera ambazo zitapunguza uzalishaji wa gesi chafu na kusisitiza upandaji wa miti. 

Source: https://www.bbc.com/news/world-africa-58614677 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *