By Khadija Mbesa
UNICEF inatoa wito wa kuzuia muongezeko wa vita na ulinzi wa Watoto wote.
Taarifa kutoka kwa Ted Chaiban, Mkurugenzi wa Kanda wa UNICEF wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini na Lucia Elmi, Mwakilishi Maalum wa UNICEF katika Jimbo la Palestina.
AMMAN / EAST JERUSALEM, 9 Mei 2021 – “Kwa siku mbili zilizopita, watoto 29 wa Kipalestina walijeruhiwa Mashariki mwa Jumuiya katika Jiji la Kale na kitongoji cha Sheikh Jarrah. Huku Watoto wane wa kipalestina wakikamatwa
“Mtoto mchanga wa mwaka mmoja alikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa. Watoto wengine walichukuliwa kwa matibabu hospitalini wakiwa na majeraha kwenye kichwa na mgongo.
“Hii inakuja wakati kukiwa na ripoti kwamba karibia watu 300 walijeruhiwa katika eneo hilo.
“UNICEF ilipokea ripoti kwamba magari ya kusaidia wagonjwa yalizuiliwa kufika mahali ili kusaidia na kuwaokoa waliojeruhiwa na kwamba kliniki ya eneo hilo iliripotiwa kugongwa na kupekuliwa.
“Watoto wote wanapaswa kulindwa kutokana na vurugu ya aina yoyote na kuwekwa mbali wako wowote, haki za familia za kuenda na kuhifadhi maeneo yao ya ibada inapaswa kuwekwa sambamba na wale waliojeruhiwa wakati huo wa vita waweze kupata msaada bila ya kizuizi chochote.
“UNICEF inahimiza mamlaka ya Israeli kuacha kutumia unyanyasaji dhidi ya watoto na kuwaachilia watoto hao wote wanaoshikiliwa. Kuzuiliwa kwa watoto ni suluhisho la mwisho na inapaswa kutumika kwa muda mfupi zaidi iwezekanavyo.
“Wakati huo huo katika Ukanda wa Gaza, sehemu za Ukingo wa Magharibi na Kusini mwa Israeli, kuna wasiwasi kuhusu kuanza tena kwa ghasia haswa katika masaa 24 yaliyopita.
“Tunatoa wito kwa pande zote zinazohusika popote walipo kuzuia ongezeko lolote na kulinda raia wote haswa watoto.”