By Khadija Mbesa
Mtaala wa Ustadi (CBC) chini ya mfumo wa 2-6-3-3 wa elimu nchini Kenya ulifunuliwa mnamo 2017 kuchukua nafasi ya mfumo wa elimu wa 8-4-4 ambao umetumikia Kenya kwa miaka 32.
shule zinajizatiti kwa bidii ili kuweza kuendeleza mfumo huu wa 2-6-3-3.
utekelezaji huu umekua changamoto dhahiri upande wa wazazi na walezi kifedha, kwani wanatumia hela nyingi kwa vitabu tu, wizara ya mkurugenzi wa nyumba ya watoto ya cheryl Childrens home ilieleza kwamba, “kuna changamoto nyingi mno, iwapo tunaweza pata wafadhili wanaosaidia kwa njia anuwai , basi itakuwa vyema mno, changamoto kubwa zaidi kwa sasa ni shida ya kuweza kupata vitabu, hususan mwanafunzi kutokubaliwa kutumia kitabu na mwenzie, na kukosa mfadhila wa kumsaidia mtoto huyo kununua vitabu, na mipango ya kukaa kwa vikundi ambapo utapata hakuna madawati ya kutosha.
mfumo huu wa CBC unaelemea sana upande wa kutumia vifaa vya digitali kwa watoto na hata kwa walimu, hili likiwa changamoto kwa watoto wa makazi duni, kwani vifaa vya kompyuta ni ghali mno.
vifaa hivi ni muhimu, maana hata ukawa unasomesha somo la kiswahili, sayansi ama hisabati, vitabu pekee haviwezi kutekeleza jukumu la kuwaelewesha wanafunzi, hii ikikusudia kutumia vifaa vya digitali kwa madai ya vitendo. hali hii ikiwa ngumu zaidi kwa shule za makazi duni, kwani wana uhaba wa vitabu na vile vile uhaba wa vifaa vya digiitali.
Je? ni jambo lipi linaweza fanywa ili linufaishe watoto hawa walio katika makaazi duni? kila mtoto ana haki ya kusoma, iwe maskini au tajiri.
kutoka kwa vitabu, hadi vifaa vya digitali, hili limekuwa changamoto dhahiri kwa wazazi wengi.