Mapinduzi ya Kisiasa nchini Myanmar

By Martha Chimilila

Mapinduzi ya kisiasa nchini Myanmar katika kipindi cha miezi mitano, yamesababisha watoto wengi kuuawa na mamia kuzuiliwa kiholela. Wataalamu wa Haki za Umoja wa Mataifa walisema michafuko ya kisiasa yanaendelea katika kipindi cha dharura za kiafya zilizoletwa na janga la Corona.

Kamati ya haki za watoto ya Umoja wa Mataifa iliripoti Ijumaa kwamba imepokea habari ya kuaminika kwamba ‘watoto 75 waliuawa na takribani 1,000 walikamatwa nchini Myanmar tangu February 1,2021

Iliundwa Kamati ya kufatilia utekelezaji wa Mkataba wa Haki za Mtoto, ambayo Myanmar ilisaini mnamo mwaka 1991. Wataalamu wa Kamati hiyo walisema “tunalaani vikali mauaji ya watoto yanayofanywa na junta na polisi”

Baadhi ya Kauli zilizotolewa na Kamati hiyo ni kama yafuatayo;

Watoto nchini Myanmar wanakabiliwa na janga la kupoteza Maisha, lililosababishwa na Mapinduzi ya kijeshi” alisema Mwenyekiti wa Kamati bwana Mikiko Otani.

Watoto wanakabiliwa na vurugu za kiholela, upigaji risasi bila mpangilio na kukamatwa kiholela kila siku” aliongezea

Wataalamu hao pia walilaani kuzuiliwa kiholela kwa watoto katika vituo vya polisi, magereza na vituo vya kizuizini vya Jeshi. Hii ilitokea wakati vyombo vya usalama kushindwa kuwakamata wazazi wao, ambao walishiriki kuandaa maandamano ya kupinga utawala wa kijeshi.

Siku ya Ijumaa, tovuti ya habari ya Myanmar Now iliripoti kuwa watoto wawili, wenye umri wa miaka 12 na 15 walikua miongoni mwa wana kijiji saba kutoka mji wa Sintgaing wa mkoa wa Mandalay, walizuiliwa na kushtakiwa kwa kosa la kuwa na vilipuzi.

Mgogoro huu ukiendelea, kizazi kizima cha watoto kiko katika hatari ya kupata matatizo makubwa mwilini, kisaikolojia, kihemko, kielimu na kiuchumi, na kuwanyima uwezo wa kupata Maisha bora hapo baadae” Mikiko Otani alielezea hofu yake.

Source: https://www.aljazeera.com/news/2021/7/17/75-children-killed-1000-detained-since-myanmar-coup-un-experts

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *